Chama hatimaye aondoka rasmi Msimbazi Julai 3, 2024

DAR ES SALAAM: NI takribani kilomita 0.6 ametumia Clatous Chama kutoka Makao Makuu ya Klabu ya Simba  Msimbazi kwenda ‘Twiga Street’ Jangwani na hatimaye ‘Magician’ huyo ameaga rasmi.
Chama anayeufanya mchezo wa soka kuonekana kama kula ice cream ya maziwa au kunywa asali huku ukiwa na smartphone ukitizama picha za Hamisa Mobeto, ametumia miaka sita kuifikisha Simba robo fainali mara nne akiwa Msimbazi.
Yanga walimtambulisha Chama siku tatu zilizopita, hata hivyo barua ya Chama imejibu sintohamu za kwanini alishindwa kutokea kwenye hafla za kula keki, na kushindwa kubadili utambulisho wake Instagram.
“Baada ya miaka sita ya furaha, majivuno na malengo, hatma zetu zilizounganishwa zinachukuwa mkondo mwingine, sina cha kuwalipa zaidi ya heshima kwa kila mmoja wenu kwa mapenzi na kuniunga mkono kwa miaka yote na hakuna atakayebadili historia tuliyotengeneza pamoja,” ameandika Chama kwenye Instagram yake.
Sasa fundi huyo wa soka atawatumikia Wananchi msimu ujao. Itoshe kusema Wanasimba wanapaswa kukubaliana na ukweli kuwa kipenzi chao kimetoka mitaa ya Msimbazi eneo la Kariakoo.

Clatous Chama alizaliwa tarehe, 18 Juni 1991, Huko Mansa, Zambia. Alianza taaluma yake ya soka katika klabu ya Zesco United mwaka 2012, ambako alishinda mataji kadhaa ya ligi Kuu ya Zambia.

Mwaka 2018, alihamia Tanzania kujiunga na klabu ya Simba, ambako aliisaidia klabu hiyo kushinda mataji ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Clatous Chama amekuwa sehemu muhimu ya timu ya taifa ya Zambia, akicheza katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Mnamo mwaka 2021, alirudi Simba baada ya kipindi kifupi cha kucheza nchini Misri na klabu ya RS Berkane.

Clatous Chama alionyesha uwezo mkubwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na Simba, akichangia katika ushindi wa klabu hiyo kwenye mechi muhimu.

Msimu wa 2020/2021 aliisaidia Simba kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, akifunga mabao na kutoa pasi za mwisho za mabao.

Uchezaji wake Simba katika mashindano hayo umemfanya kuwa mmoja wa wachezaji muhimu na maarufu katika soka la Afrika Mashariki.

Chama alionekana kuwa na ushirikiano mzuri na wachezaji wenzake wa Simba, jambo lililowezesha klabu hiyo kufanya vizuri katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *