Showing posts with label UDAKU. Show all posts
Showing posts with label UDAKU. Show all posts

Monday, August 19, 2019

PICHA: Mh Kikwete Alichomuambia Harmonize

PICHA: Mh Kikwete Alichomuambia  Harmonize

PICHA: Mh Kikwete Alichomuambia  Harmonize

PICHA: Mh Kikwete Alichomuambia  Harmonize

PICHA: Mh Kikwete Alichomuambia  Harmonize
KUTOKA KWA HARMONIZE "Jana Nilipata Nafasi Ya Kujumuika Katika Dhifa Ya Taifa Ilioandilia Na Raisi Wetu Kipenzi Doctor John Pombe Magufuli statehouse Jijini Dar es salaam Naamini Nilikuwa Pale Kuwakilisha Vijana Wengi Walio Mtaani Na Wenye Ndoto...!!! 🙏🙏 Hakika ilikuwa Bahati Kwangu Kukutana Na Viongozi Wa Ngazi Za Juu Kabisa Kila Nilie kutana Nae Pale Ndani Alinipongeza Sana..!! Na Kuniambia wanajivunia Uwepo Wangu Katika Hili Taifa Tukufu Ilinipa Moyo Na Somo La Kwamba Kupitia Kipaji Chako Au Kazi Yako Hiyo Hiyo ifanye Kwabidi...!!! Utatimiza Kila Aina Ya Ndoto Yako...!!! Na Kupewa Kila Aina Ya Heshima..!! Kijana Mwenzangu Chukua Hiyo
Lakini Mwishoni Kabisa Nikakutana Na Swahiba former President D.R Jakaya Mrisho Kikwete Tulifurahi Sanaa Akaniambia Wewe Sasahivi Sio Msani Tena Wewe Ni Mwanamuziki Ni Wakati Wa Kuifanya Tanzania Iendele Kuwa proud Na Wewe Watanzania Woteeee Wanakupenda Na Wana kusupport Go go go.....!!! Nami Nikamwambia Sitoweza Kuwaangusha Na Sitoweza kuku Disappoint Yani Subiri Tuu Uone Hili Movie Linavyoenda...!!! Akacheka Sana mwisho Akaniambia Mimi Nakutakia Kila La Heri...!!! Love You Dady ❤❤" - @harmonize_tz

Saturday, August 17, 2019

Jinsi ya Kudhibiti Hasira

Jinsi ya Kudhibiti Hasira
Inaweza tokea mwenzi wako akasema au kufanya jambo ambalo linakukasirisha, na unajaribu kufungia hasira yako asijue. Lakini mwenzi wako anahisi kwamba amekukosea kwa njia fulani, kwa hiyo anaanza kukuhoji. Kufanya hivyo kunakukasirisha zaidi. Unaweza kufanya nini ili udhibiti hasira yako chini ya hali kama hizo?
Mambo unayohitaji kuyajua
Kukasirika kunaweza kudhuru afya yako.Utafiti unaonyesha kwamba hasira isipodhibitiwa inaongeza hatari ya kupanda kwa shinikizo la damu, kupata ugonjwa wa moyo, kushuka moyo, na matatizo ya umeng’enyaji. Pia, hasira imehusianishwa na matatizo ya kukosa usingizi, kuongezeka kwa mahangaiko, matatizo ya ngozi, na kiharusi.
Kufungia hasira kunaweza kukudhuru piaUkiendelea kufungia hasira inaweza kuwa kama ugonjwa ambao unakuumiza kutokea ndani. Kwa mfano, unaweza kuwa na mtazamo wa kuona tu mambo mabaya na kuchambua-chambua. Roho kama hiyo inaweza kufanya iwe vigumu kuishi pamoja nawe na kuathiri sana ndoa yako.
Mambo unayoweza kuyafanya
Tafuta sifa nzuri za mwenzi wako.Orodhesha mambo matatu unayopenda kumhusu mwenzi wako. Wakati ujao utakapokasirishwa na kitu ambacho mwenzi wako anafanya, fikiria kuhusu sifa hizo ulizotaja. Huenda hilo likakusaidia kudhibiti hasira yako.
Mke mwenye shughuli nyingi anafikiria jinsi mume wake humsaidia kufanya kazi za nyumba, kumsikiliza, na kumjali anapokuwa mgonjwa
Sitawisha mtazamo wa kusamehe. Kwanza, jaribu kuona mambo kwa kutegemea maoni ya mwenzi wako. Hilo litakusaidia uwe na hisia kama za mwenzi wako​. Jiulize je, jambo linalonifanya nikasirike ni kubwa sana hivi kwamba siwezi kusamehe?’
Eleza hisia zako kwa fadhili na busara. Jieleze ukitumia neno “mimi.” Kwa mfano, badala ya kusema, “Wewe unakosa ufikirio unapokosa kunipigia simu na kunijulisha mahali ulipo,” sema “Mimi huwa na wasiwasi saa zinaposonga na sijui ikiwa uko salama.” Kueleza hisia zako kwa upole kunaweza kukusaidia kudhibiti hasira yako.
Tokeo la picha la couples talkingSikiliza kwa heshima. Baada ya kujieleza, mruhusu mwenzi wako azungumze bila kumkatiza. Mwenzi wako anapomaliza kuzungumza, rudia kwa maneno machache kile alichosema ili uone ikiwa umemwelewa vizuri. Tendo dogo la kusikiliza linaweza kuchangia sehemu kubwa katika kukusaidia kudhibiti hasira yako.

Jinsi ya kuishi na mtu mwenye wivu katika mahusiano ya kimapenzi

Jinsi ya kuishi na mtu mwenye wivu katika mahusiano ya kimapenzi

Mtu mwenye mafanikio kwenye mapenzi ni yule anayeamini katika saikolojia ya kujitambua. Hapa nikupe msisitizo kuwa ni lazima ujitambue ili uweze kuwa bora kwenye mapenzi. Kama hujitambui, maana yake hutajua ulitendalo.

Ikiwa utashindwa kujua ulitendalo, wewe utageuka kuwa kero kwa mwenzi wako. Ukifikia hatua hiyo, unadhani ni nani anaweza kukuelewa? Ni vema ujijue, ujifahamu kasoro na uimara wako katika uhusiano wako. Kama unamfurahisha au kumchukiza, yote yanafaa kugota ndani ya kichwa chako.

Je, una wivu? Hilo unapaswa kulitambua kwa sababu lipo ndani yako. Bahati mbaya ni kwamba watu wanakuwa na wivu wa kupitiliza lakini wakiambiwa wanakuwa wakali. Wanadai wanasingiziwa.

Ni vizuri ukatambua upungufu ulionao kabla ya kuelezwa na mtu wa pili.

Wivu wako umekugharimu mara ngapi? Makala haya yanatosha kuwa tiba yako ya kudumu. Pengine hujawahi kukaa, ukatafakari na kugundua kuwa wivu wako unakupeleka njia isiyo sahihi kimapenzi, hapa chini kuna mambo  ambayo ni muongozo madhubuti.

Jifunze kwa watu wengine.
Mara nyingine ni rahisi kugundua kuwa unafanya makosa baada ya kuwaona wengine na kujifunza kutoka kwao. Hivyo basi, jaribu kuwaangalia watu wengine walio kwenye uhusiano. Fuatilia mtindo wao wa maisha, mafanikio yao kisha ujitazame wewe.

Bila shaka hapo ulipo, utakuwa umeshawahi kujionea wanaume na wanawake wenye wivu, jinsi wanavyotenda mambo yao, wanavyoudhi na kuchukiza kwenye uhusiano. Kama ndivyo, basi hilo ni somo kwako kwa kuepuka yale yaliyowafanya wachukize.

Inawezekana ukawa umeona kupitia kwa macho yako au umesimuliwa. Muhimu kutambua ni kwamba hulka za wivu, hususani unapozionesha mbele za watu wa pembeni ni mbaya. Kwa mantiki hiyo, kama utaweza kutambua na kuelewa alama za wivu, sina shaka kuwa utakuwa unaweza kujua jinsi ya kuishi katika mazingira salama.

Mpe nafasi
Kumbana mwenzi wako haina maana ndiyo utamfanya adumishe uaminifu kati yenu. Jifanye kama mtu usiyejali, muache atoke na marafiki zake. Inaweza kuwa tatizo endapo ataona unamnyima uhuru anaoutaka. Anahitaji nafasi ya kufurahi na marafiki zake, unambana kwa nini?

Akilini kwako lazima ukubali kwamba mwenzi wako ni mtu mzima na anajitambua, kwa hiyo uhuru utakaompa, utawezesha yeye kujiamini zaidi na kuheshimu uaminifu wako kwake. Kisaikolojia, mwenzi wako akigundua unamuamini, naye huzidisha upendo.

Vizuri pia kutambua kuwa wivu hukua zaidi pale mmoja anapokuwa na hisia kwamba mwenzi wake anasaliti. Kama upo kwenye uhusiano wenye afya, huhitaji kusumbuliwa na mawazo mabaya. Endapo utashindwa kuondoa wingu la shaka ndani yako, kaa ukijua kuwa unajiharibia.

Ongeza uaminifu.
Mojawapo ya dawa nzuri ya kukabiliana na wivu ni kuongeza kiwango cha uaminifu. Muamini mwenzi wako na utaona jinsi mambo yatakavyokwenda. Tunza akilini kwamba kutengeneza uhusiano imara na wenye mafanikio, huhitaji kiwango kikubwa cha uaminifu.

Amini kuwa mwenzi wako atafanya mambo sahihi hata kama wewe hutakuwepo. Muamini kuwa anajitambua, kwa hiyo hatakuwa na muda mchafu wa kutenda maovu kwa kigezo kwamba haupo. Ana akili timamu, akiamua kutenda ‘uwaluwalu’, hashindwi hata kama utakuwepo.

Kwa kawaida, anaweza kuwepo mtu ambaye atakufanya usimuamini mwenzi wako hata kidogo. Inawezekana akakujengea picha kutokana na maneno ya zamani au matukio yaliyopita. Je, unaona wivu kwa sababu umeambiwa mpenzi wako aliwahi kutoka na watu wawili tofauti kabla yako?

Wivu wa nini? Kwa nini maneno hayo yakuchanganye akili? Je, ulimkuta akiwa mbumbumbu wa mapenzi na hajawahi kutoka na yeyote? Kumbe utabaini kuwa historia ya mwenzi wako haina maana inayokubalika kwenye uhusiano endelevu.

Wanasema shetani wa jana, leo anaweza kuwa malaika. Vilevile malaika wa leo kesho anaweza kuwa shetani. Inawezekana hao ulioambiwa alitoka nao walimtenda ndiyo maana hakuwapa nafasi ya kudumu lakini wewe umepata fursa hiyo kwa sababu unakidhi mahitaji yake.

Friday, August 16, 2019

Wadada Mjue Hili Swali la “Utakuja Lini Kwetu Kujitambulisha?” Linavunja Mahusiano Mengi Sana

Wadada Mjue Hili Swali la “Utakuja Lini Kwetu Kujitambulisha?” Linavunja Mahusiano Mengi Sana

Tatizo kubwa la wadada wakisgafikisha miaka 28 kuendelea, ukimtongoza anafikiri kuwa unataka kumuoa, mara ghafla anaanza kukupa mipango ya miaka kumi ijayo mpaka unaanza kuboreka. Mtu hata miezi mitatu hamjamaliza ashaanza kukuuliza “Kwetu unakuja lini?” Dada zangu nije kufanya nini? Kwamba kuna staili ambazo huwezi kunipa mpaka nije kwenu? Hapa ndipo wadada wengi wanaanza kuboa, kwakua ukimuambia kuwa nikama wanalazimishia ukajitambulishe wakati wewe unataka kustarehe.

Nafasi za Kazi Bonyeza HAPA

Maswali yanakua mengi, visirani vinakua vingi mpaka mwanaume unaanza kuwaza “Hivi kama miezi mitatu hivi ananuna mpaka mdomo unanuka kisa tu sijapokea simu yake nitaweza kuishi naye mpaka afe huyu?” Dada zangu mimi nawalewa, lakini unaja wako umekula huko na X wako, mmekaa miaka 7 unampikia na kumpakulia hajaja hata kwenu kuangalia TV, mimi nimejuana na wewe miezi mitatu unataka nikajitambulishe?

Unataka mwanaume akajitambulishe kwenu, mtu hata X wake hajaachana naye vizuri, mwingine alichawa anasubiri akama ataerudiwa au la unataka akajitambulishe kwenu halafu? Najua umri umeenda lakini punguza kasi, tena mwanamke unatakiwa kushtuka umekaa na mwanaume miezi mitatu anataka kuja kwenu kujitambulisha, narudia unatakiwa kushtuka kwani mara nyingi wa namna hiyo naye ni kichomi tu hivyo chunguza kidogo.

Hili swali la “Utakuja lini kwetu kujitambulisha?” Linavunja mahusiano mengi sana, wanawake wanakua na wasiwasi sana wa kuachwa mwanaume akishindwa kulijibu, kibaya Zaidi nikuwa mwanamke anakua na maswali mengi, wasiwasi ambao unageuka na kuwa kisirani, kwa namna hiyo mwanaume anakuchoka, hata kama una mzuka wa kuolewa acha kuuliza kwanza hembu msome mwanaume na si kukimbilia kuuliza wakati unaona matendo yake hayaelekei!

Nafasi za Kazi Bonyeza HAPA

Monday, August 12, 2019

Sifa za wanawake wanaopendwa

Sifa za wanawake wanaopendwa
Mara nyingi wanaume wengi hupenda wanawake wenye sifa zifuatazo katika mahusiano ya kimapenzi;

Wenye msimamo
Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.

Wapenda usawa
Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50.

Wenye urafiki ndani yake
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani.

Wanaojitegemea
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina naomba vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja.

Wanaoridhika
Wanawake ambao hulidhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.

Dalili za mwanamke asiyekupenda kwa dhati

Dalili za mwanamke asiyekupenda kwa dhati
Unapokuwa  kwenye mahusiano ya kimapenzi  mwanamke ambaye hakupendi kwa dhati basi utamgundua kwa dalili zifuatazo;

1. Hataki kuambata na wewe katika matembezi na ikitokea anakuwa mtu wa masharti mara akuambie tangulia nakuja au pengine kutembea nawe kwa umbali.

2. Anapata kigugumizi kukutambulisha kwa rafiki zake na ndugu na inapotokea amebanwa hafikishi ujumbe kwa kiwango timilifu.

3. Haoneshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleao, kwake ni kufuja mali na anapokosa kupewa pesa ni mwepesi kulalamika na wakati mwingine kununa kabisa.

4. Anaahilisha mara kwa mara kukutana na wewe tena bila kukueleza sababu za msingi Au kukutungia uongo wa dhahili na kuusisitiza bila kuona aibu.

5. Anapokuwa akitoa maelezo ya mwanaume amtakaye sifa zake zinakuwa hayalingani na wewe. Anaweza kukuambia napenda kuishi na mwanaume mwenye gari au mwenye mwili mkubwa, sifa ambazo wewe huna!

6. Hacheki kwa furaha hata kama ukimchekesha haoneshi furaha ya moyoni. Tena mara nyingine anakuwa mkimya na mshiwishi mkubwa wa kuachana kutoka kwenye matembezi yenu ya jioni. “Aaah, mi nimechoka narudi nyumbani”

7. Anajaribu kukuunganisha na wanawake wengine na haoni vibaya anaposikia unamfukuzia mwingine badala yake anakutia moyo wa kuendelea na usaliti wako. Hana wivu kabisa.

8. Hajuti anapokukosea, mwepesi wa kujitenga, kutokuzungumza nawe na mwingi wa kukusukumia makosa hata kama yeye ndiye aliyekukosea.

9. Msambazaji wa habari za udhaifu wako na mtu asiyekusifia mbele za wenzake. Si balozi mwema kwa familia yake, haishi kukuponda mbele ya wazazi na ndugu zake.

10. Mwepesi wa kupokea na si wa kutoa mmiliki wa mali zako na mkumbatiaji wa mali zake pia. Msiri wa mipango yake na mtu anayependa kujua zaidi ya kwako kuliko wewe kujua yake.

HABARI HIZI ZOTE UTAZIPATA KATIKA APP YETU YA MUUNGWANA BLOG  BOFYA HAPA KU-DOWNLOAD SASA ..