Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

KMC INA SABABU NNE ZA KUITOA AS KIGALI1. Ubora wa kikosi
Hili halina ubishi kabisa.. Miongoni mwa timu chache zilizofanya usajili wa maana msimu huu ni KMC.. Imemsajili aliyekuwa mfungaji bora wa Mwadui kwa msimu uliopita, Salim Aiyee.. Ikamsajili aliyekuwa mfungaji bora wa Kagera Sugar, Ramadhani Kapera, wa Ndanda, Vitalis Mayanga na wengine kibao. Imechukua viungo wa nguvu kama Jean Mugiraneza na Kenny Ally.. Kwa kifupi timu imeiva.

2. Uwezo wa Mayanja 
KMC iko chini ya mikono salama ya kocha Mganda, Jackson Mayanja.. Kocha mwenye historia tamu hapa nchini. Mayanja aliwahi kuifanya Kagera Sugar kuwa ya kutisha.. Aliwahi kuifanya Simba kupata matokeo ya kustaajabisha. Hakika akili yake imebeba dhamana kubwa ya mchezo huu. 
3. Sare ugenini
Kwa kupata tu sare ugenini, KMC imethibitisha kuwa ni timu ya ushindani.. Imethibitisha kuwa ni timu bora.. Siyo tu kwamba ilipata sare ugenini, hapana, ilicheza pia kandanda safi. KMC ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga.. Kama KMC ilikuwa bora pale Kigali, itashindwaje kuitoa As Kigali hapa? Haiwezekani.

4. Mipango ya viongozi.
Tayari KMC imekuwa na mipango imara nje ya uwanja.. Viongozi wake wakiongozwa na Meya Sitta wamekuwa imara kimkakati kuhakikisha wanashinda mechi hii.. Kwanza, wamehakikisha wachezaji wako kwenye mazingira mazuri.. Pili wametoa motisha ya kutosha kwa wachezaji wao kuhakikisha kuwa wanajituma zaidi na kupata ushindi.. KWETU MASHABIKI
Kazi yetu mashabiki ni moja tu, kuhakikisha tunakwenda kwa wingi Uwanja wa Taifa Ijumaa hii kuishangilia KMC..Kiingilio ni buku mbili tu... Kumbuka kuwa KMC inafanya jambo la kitaifa. 
KMC tunasema

USM Alger yatembeza bakuli

USM Alger yatembeza bakuli

USM ALGER inayoshiriki ligi kuu nchini ALGERIA na mashindano ya kimataifa barani africa CAF imekumbwa na ukata wa pesa na kushindwa kulipa mishahara ya wachezaji tangu mwezi wa 3.

Vile vile klabu imeshindwa kulipa ada ya usajili kwa wachezaji wapya msimu huu huku menejiment ya klabu hiyo ikijitahidi kutatua jambo hilo la ukata kutoka kwa wadau mbalimbali na taarfa za ndani zinadai kuwa kuna uwezekano kujitoa mashindano ya CAF msimu huu endapo haili itaendelea hivi hivi hata kama watafuzu hatua ya makundi .

Klabu pia ilikuwa kwenye hati hati ya kukosa nauli na mahitaji muhimu kuifuata CS CASSABLANCA kwa ajili ya mpambano ila wadau na wapenzi wa klabu hyo wamejichanga na kufanikisha kupatikana kwa fedha zitakazoiwezesha klabu hiyo kukidhi taratibu nzima kwa ajili ya mchezo huo.

Haya ni mapito na magumu yoyote yanaweza mtokea tuungane tusitofautiane na kuweka makundi hii ni klabu yetu sote" maneno ya mkurugenzi klabu hiyo HOSSAM
MASHABIKI WA SIMBA WAONYESHA UUNGWANA

MASHABIKI WA SIMBA WAONYESHA UUNGWANA

Tokeo la picha la MASHABIKI WA SIMBA
Juzi video ya mashabiki wa Yanga mkoani Kilimanjaro ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii wakichana jezi ya klabu ya Simba tukio ambalo lilikemewa vikali na familia ya soka nchini ukiwemo uongozi wa Yanga ambao uliwataka mashabiki wao kuacha tabia ya kufanya uhasama kwenye ushabiki

Lakini mwenzao wa Simba wamewafundisha kuwa Simba na Yanga ni watani tu na hakuna uhasama wowote baina yao baada ya hapo jana baadhi ya mashabiki kumkaribisha mshambiki wa Yanga aliyekuwa akishangilia Azam Fc kukaa jukwaa la Simba


Tukio hilo lilitokea kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Azam Fc na kumfanya shabiki huyo ajikute kwenye wakati mgumu baada ya kupigo hicho cha Azam

Watatu Yanga Kuwakosa Township RollersSasa rasmi golikipa namba moja wa klabu ya Yanga, Farouk Shikalo, Beki Mustapha Selemani na Mshambuliaji David Molinga Ndama Falcao wataikosa mechi ya marudiano ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana mchezo ambao utachezwa jumamosi ya August 24.

Sababu kubwa ni kuchelewa kupata Leseni zao kutoka CAF ni hii imetokana na klabu ya Yanga kuchelewa kutuma ITC zao CAF. Sio Yanga tu hata KMC nayo inawakosa baadhi ya wachezaji wake wapya na CAF imesema wachezaji hao wataruhusiwa kucheza kuanzia michezo ya raundi ya kwanza.
Matokeo Ya Michezo Ya Ligi Mbalimbali Zilizopiga Jana Ulaya, Na Msimamo Wa Ligi Kuu England.

Matokeo Ya Michezo Ya Ligi Mbalimbali Zilizopiga Jana Ulaya, Na Msimamo Wa Ligi Kuu England.

Image

EPL

FT: Sheffield United 1-0 Crystal Palace
⚽ Lundstram 47'

FT: Chelsea 1-1 Leicester City
⚽ Mount 7'
⚽ Ndidi 67'

LaLiga

FT: Atlético Madrid 1-0 Getafe
⚽ Morata 23'

FT: Deportivo Alavés 1-0 Levante
FT: Espanyol 0-2 Sevilla
FT: Real Betis 1-2 Real Valladolid


CoppaItalia - Round 3

FT: Perugia 2-1 Brescia
FT: Fiorentina 3-1 Monza
FT: Hellas Verona 1-2 Cremonese
FT: Cagliari 2-1 Chievo
FT: Udinese 3-1 Südtirol
FT: Sassuolo 1-0 Spezia
FT: SPAL 3-1 FeralpiSalò
FT: Lecce 4-0 Salernitana
FT: Pisa 0-3 Bologna
FT: Crotone 1-3 Sampdoria


Ligue1

FT: Rennes 2-1 PSG
⚽ Cavani 36'
⚽ Niang 44'
⚽ Del Castillo 48'

FT: Saint-Étienne 1-1 Brest
FT: Reims 0-0 StrasbourgBundesliga

FT: Eintracht Frankfurt 1-0 Hoffenheim
FT: Union Berlin 0-4 RB Leipzig

Msimamo Wa Ligi Kuu England Mara Baada Ya Kumalizika Kwa Michezo Ya Wikendi Hii.
Image
MO AZUIA PRESS YA HAJI MANARA KESHO

MO AZUIA PRESS YA HAJI MANARA KESHO

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Simba ambaye ni mwekezaji wa timu hiyo, Mohammed Dewji, amezuia mkutano wa msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara na waandishi wa habari uliokua umepangwa kufanyka kesho.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka msemaji huyo aliyoiposti kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ilisomeka kama ifuatavy

Boss wangu (Mo Dewji) amezuia press yangu ya kesho na huyu ni mtu ninayemuheshimu sana ,niwahakikishie nitaendelea kufanya kazi katika Club hii ya Simba ninayoishabikia sana'

"Sote sisi nterest yetu ni Simba,hakuna kurudi nyuma hadi Wanasimba tutimize malengo yetu, Vita yetu sasa tuhamishie kwa Wabangu bangu.. Na tutawaambia kwa sauti kubwa
Welbeck Atuma Ujumbe Huu Kwa Arsenal

Welbeck Atuma Ujumbe Huu Kwa ArsenalStraika wa zamani wa zamani wa klabu ya Arsenal, Danny Welbeck ametoa shukurani zake za dhati kwa klabu hiyo ambayo ameitumikia kwa kipindi cha miaka mitano akitanabaisha kua alionyeshwa upendo wa kipekee.

Aidha amepeleka shukurani zake pia kwa wapenzi na mashabiki wa washika mitutu hao wa Jiji la London, Arsenal na kusema kuwa hawezi kuusahau ushirikiano waliompatia katika kipindi chote alichua nao.

Straika huyo ambaye amewahi kukipiga kunako vilabu tofautitofauti vikiwemo Preston na Manchester United kwa sasa amejiunga na klabu ya Watford akitokea Arsenal..


Image

Yanga Yaitandika AFC Leopards Huko Arusha, Zahera Asema Walienda Kupoteza Muda..Mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliowashirikisha mabinwa wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania, Yang SC umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi mwembamba wa goli 1 - 0 dahidi AFC Leopards.

Alikua ni nahodha, Papy Tshishimbi aliyewaamusha Wananchi waliofurika katika dimba la Shekhe Amri Abeid kwa kuzamisha kimiani mpira wa kona uliopigwa na Patrick Sibomana mnamo dakika 83' na kuwaweka Wananchi kifua mbele.

Mara baada ya mchezo huo kumalizika kocha mkuu wa klabu hiyo Mkongomani Mwinyi Zahera atupia lawama zake kwa waandaaji wa michezo yote ya kirafiki ambayo timu yake imeicheza huku lawama kubwa zikiwa juu ya viwanja huku akisema kambi yake ya Arusha na Kilimanjaro ni kupoteza Muda.

"Tuna mchezo mgumu na muhimu wa marudiano dhidi ya Township Rollers, nahitaji muda kuiandaa timu lakini tunakuja kupoteza muda huku Moshi na Arusha. . tunacheza na Polisi kisha AFC katika viwanja vibovu hakuna jambo la maana tulilofaidika nalo hii ziara tungeweza kuifanya muda mwingine sio huu. . jambo la msingi nna matumaini ya kwenda kufanya vema kule Botswana kwa maana tutacheza katika uwanja mzuri" 
-Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Zahera Mwinyi.

Simba Nooma Yajipigia Matajiri Wa Dar, Azam Fc Na Kutwaa Ngao Yao Ya Jamii Taifa

MECHI ya 12 leo Uwanja wa Taifa imekamilika na umezalisha mabao mengi kuliko mchezo wowote tangu kuanza kwa michuano hii mwaka 2001.

Sasa Simba imefikia hatua ya Yanga ambao walitwaa mataji hayo mara tano na leo wamefikia hatua ya kutwaa mataji matano.

Azam ambayo imecheza michuano hii mara sita imetwaa taji hilo mara moja sawa na Mtibwa Sugar na iliifunga Yanga kwa penalti.

Hivyo kwa sasa ni rasmi Pazia la Ligi Kuu Bara limefunguliwa kwa Simba kutwaa ngao yao ya jamii ambayo msimu uliopita walitwaa mbele ya Mtibwa Sugar kwa ushindi wa mabao 2-1.

Mabao ya Simba yamefungwa na Sharaf Shiboub ambaye alipachika mabao 2 dakika ya 17 na 21 la tatu limepachikwa na Chama dakika ya 56 na msumari wa mwisho umepachikwa na Kahata dakika ya 78.

Yale ya Azam yamepachikwa na Idd Chilunda dakika ya 13 na Frank Domayo dakika ya 78.

FT: Simba 4-2 Azam Fc


Ngao ya Jamii mpira umekamilika
Simba 4-2 Azam FC

UWANJA wa Taifa kwa sasa mchezo kati ya Simba na  Azam FC umekamilika kwa Simba kushindwa kwa mabao 4-2.

Mabao mawili yamefungwa na Shibob dakika ya 17 na 21 na la tatu limepachikwa na Chama dakika ya 56 na la nne limepachikwa na Kahata dakika ya 85 huku Azam FC bao la kwanza likifungwa na Idd Chilunda dakika ya 13 na la pili Frank Domayo dakika ya 78.

Azam FC walianza kuandika bao moja matata sana kupitia kwa Idd Chilunda dakika ya 13 kabla ya Shibob kusawazisha kwa kichwa dakika ya 16 kwa upande wa Simba na kupachika la pili dakika ya 21.