Showing posts with label BREAKING. Show all posts
Showing posts with label BREAKING. Show all posts

Wednesday, August 14, 2019

Harmonize Avunja ‘mwiko’ Wa Wcb, Amfuata AlikibaTETESI za Msanii Harmonize kuondoka katika lebo ya WCB zimeendelea kutikisa katika mitandao ya kijamii hapa Bongo hasa baada ya Harmonize kufuta neno ‘Signed Under WCB Label’ kwenye Ukurasa wake wa Instagram.

Harmonize ameendelea kuwaaminisha watu kuwa huenda akaondoka au ameshaondoka WCB hasa baada ya kuendelea kufanya mabadiliko kwenye kurasa zake za Mitandao ya kijamii.

Kitu kingine kilichowaaminisha watu ni kitendo chake cha kuamua ‘Kumfollow’ Alikiba kwenye akaunti yake ya Instagram kitendo ambacho hakuwahi kukifanya kwa muda wote akiwa WCB.

Alikiba na Diamond Platnumz wamekuwa wapinzani wa kimuziki kwa muda mrefu na wasanii wote wa WCB hawajaifollow akaunti ya Alikiba isipokuwa Harmonize pekee ambaye ameamua kumfollow hivi karibuni.

Majina ya waombaji waliohakikiwa kikamilifu na Bodi ya Mikopo HESLB 2019/20


RITA uhakiki , RITA Tanzania, RITA majibu ya uhakiki, RITA Login, RITA verification, RITA makao makuu, RITA Contacts, RITA Application, RITA uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa, RITA veti vya kuzaliwa

THE LIST OF STUDENTS VERIFIED FOR HESLB LOAN APPLICATIONS 2019/2020

Aim
The Registration Insolvency and Trusteeship Agency (RITA) aims at effective and efficient management of information on key life events, incorporation of trustees, safeguarding properties under trust, of deceased persons, insolvents, and minors to enable the law to take its course.

Historical Background

RITA was officially launched on the 23rd June 2006 and replaces what was known as the Administrator Generals Department in the Attorney Generals Chambers, Ministry of Justice and Constitutional Affairs. It is an Executive Agency under the Attorney Generals Chambers in the Ministry of Justice and Constitutional Affairs.

DOWNLOAD IN PDF BELOW

MAJINA YA WAOMBAJI WALIOHAKIKIWA KIKAMILIFU

Saturday, August 10, 2019

VIDEO: Angalia Watu wakichota Mafuta Kabla ya Moto Kulipuka Morogoro


Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kabla ya gari hilo kushika moto na kulipuka katika ajali iliyopelekea vifo vya watu zaidi ya 60 mjini Morogoro..Lori la Mafuta laua Watu 57 Morogoro

 Lori la Mafuta laua Watu 50 Morogoro

Morogoro. “Inasikitisha”. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya lori la mafuta ya petroli kupinduka eneo la Msamvu mkoani Morogoro na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta hayo.
Tukio hilo limetokea leo Jumamosi Agosti 10, 2019 ambapo Mwananchi limefika eneo hilo na kushuhudia miili iliyoungua ikiwa imelazwa pembeni ya barabara ya  Dar es Salaam-Morogoro wengi wakiwa ni madereva bodaboda na mamalishe wanaofanya shughuli zao hapo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema karibu watu 57 wamepoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea saa mbili asubuhi.

Ajali hiyo imetokea umbali wa mita 200 kutoka kituo kikuu cha mabasi Msamvu ukitokea Dar es Salaam.

Baadhi ya mashuhuda wamelieleza Mwananchi kuwa baada ya lori hilo kupinduka, watu walianza kuchota mafuta hayo.

Wamesema mmoja wa waliokuwa wakichota mafuta hayo alikuwa akivuta sigara, kwamba ndio chanzo cha mlipuko huo.

Pia Soma

Saturday, January 26, 2019

Mama Amuua Mtoto Kisa Wivu Wa Mapenzi Kwa Mumewe

  Mama Amuua Mtoto Kisa Wivu Wa Mapenzi Kwa Mumewe
MWANAMKE mkazi wa Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kumkata na kisu shingoni mwanawe wa miezi sita, kutokana na ugomvi baina yake na mumewe kutokana na wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Augustino Senga akithibitisha kutokea kwa tukio hilo alisema tukio hilo limetokea Januari 20, mwaka huu, majira ya saa 12 jioni katika mtaa wa Kisimani kata ya Endiamtu wilaya ya Simanjiro mkoani humo.

Kwa mujibu wa Kamanda, Cecilia Paschal (29) mkulima na mkazi wa Mtaa wa Kisiwani, aligundulika kumuua mwanaye wa kumzaa, Frola Theophil kwa kumchinja na kumkata na kisu shingoni na baada ya kutenda tukio hilo alimeza dawa za hospitali ili aweze kujiua.

Chanzo cha tukio hilo, Kamanda Senga alibainisha kuwa ni wivu wa mapenzi kwani kabla ya tukio hilo inasemekana alikuta namba ya simu ya mwanamke iliyokuwa inampigia mume wake mara kwa mara.

Kutokana na hali hiyo, Januari 19, Cecilia na mumewe waliingia katika ugomvi mkubwa jambo lililosababisha mwanamume huyo kuondoka na kutorejea nyumbani kwake hadi baada ya kujulishwa tukio hilo.

“Taarifa zilitufikia mapema kutoka kwa majirani na watoto wake, Cecilia aliokolewa baada ya kukimbizwa katika Kituo cha Afya Mirerani. Kwa juhudi za madaktari alitapishwa na afya kurejea katika hali ya kawaida” amesema Senga.

Senga amekemea kitendo hicho kuwa ni kibaya na cha kusikitisha kwani mtoto huyo hakuwa na hatia na ameuawa kikatili kwa sababu ya mahusiano mabaya ya wazazi hao na kwamba hatua stahiki zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.

Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya wilaya kwa uchunguzi na kwamba mtuhumiwa ameshikiliwa na yupo kituo cha afya cha Mirerani akipatiwa matibabu.

Tanzia: Muigizaji Mama Abdul afariki Dunia


Msanii wa Maigizo, Salome Nonge (Mama Abdul) amefariki dunia.
Mama Abdul alishawahi kuigiza filamu ya KIGODORO 'kantangaze'  iliyoandaliwa na Zamaradi Mketema.

Mtangazaji, Zamaradi kupitia ukurasa wake wa Instagramu ameandika "Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa SALOME NONGE maarufu kama MAMA ABDUL."

"Kwa wasiomfahamu kama uliwahi kuangalia filamu ya KIGODORO 'kantangaze' nilibahatika kufanya nae kazi enzi za uhai wake, lakini pia kwa ambao hawajabahatika kuona filamu hiyo unaweza kumuona kupitia tamthilia ya MWANTUM kwenye stesheni ya Magic Swahili DSTV," aliandika Zamaradi huku akimalizia hiv; MUNGU amuweke mahala pema peponi Mama Abdul' Inalillahi wainailaihi Rajiun'

Kwa upande wake mama yake mzazi Monalisa ambaye anajulikana kama Natasha Mamvi ameandika  TANZIA;RAFIKI YANGU KIPENZI.MZAZI MWENZANGU.MWIGIZAJI MWENZANGU SALOME NONGE (MAMA ABDUL) AMEFARIKI. NI PENGO AMBALO HALITAZIBIKA KAMWE.RIP MAMA ABDUL.

Naye Monalisa ameandika," Mama Abdul Jamani, Pumzika kwa amani tutakukumbuka daima."

Joti naye ameandika R.I.P Mama Abdull.Mimi mwanao Sina cha kuongea zaidi ya kukuombea upate mwanga wa milele, Pumzika kwa amani mama."

Friday, January 25, 2019

Chatu Aokolewa Baada ya Kuzidiwa Nguvu na Kupe Nchini Australia

Wakamata nyoka nchini Australia wamemnusuru chatu ambaye alikuwa amevamiwa na mamia ya kupe.
Chatu Aokolewa Baada ya Kuzidiwa Nguvu na Kupe Nchini Australia
Mnyama huyo ambaye alikuwa mgonjwa alifunikwa kabisa na kupe hao, na alikutwa ndani ya bwawa la kuogelea katika eneo la Gold Coast jimboni Queensland.
Mtaalamu wa kunasa nyoka alimtoa nyoka huyo kwenye bwawa na kumkimbiza katika hospitali ya wanyama kwa matibabu.
Madaktari wa wanyama waliondoa kupe zaidi ya 500 kutoka kwenye mwili wa nyoka huyo. Tony Harrison, ambaye ndiye alimnusuru nyoka huyo ameiambia BBC kuwa inatarajiwa nyoka huyo atapona kabisa.
Chatu Aokolewa Baada ya Kuzidiwa Nguvu na Kupe Nchini Australia
Bw Harrison anaamini kuwa nyoka huyo alikuwa akijaribu kuwazamisha kupe hao kwenye maji ili ajinusuru.
"Bila shaka [chatu huyo] hakuwa na raha kabisa," amesema.
"Uso wake wote ulikuwa umevimba na ulikuwa umefunikwa na kupe waliokuwa wakimnyonya."
Amesema kumyanyua nyoka huyo ilikuwa ni kama "kubeba begi la marumaru ambazo zilikuwa zikitembea kwenye mkono wangu".
Nyoka kwa kawaida huvamiwa na kiasi kidogo cha kupe na wadudu wengine mwituni, amesema Profesa kutoka Chuo Kikuu cha Queensland.
Hata hivyo, mtaalamu huyo anasema kuvamiwa na kundi kubwa la wadudu hao inaashiria kuwa nyoka huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi yaliyotokana na joto kali ama ukame.
"Ni dhahiri kuwa alikuwa anaumwa mpaka akashindwa kujilinda kabisa. Sidhani kama angelipona iwapo asingeliokolewa na kupelekwa kupatiwa matibabu," Profesa Fry ameeleza.
Mwokozi wake, Bw Harrison baadae akaeleza kuwa nyoka huyo aliyepewa jina la Nike alipata maambukizi japo sasa "anaendelea vyema".
"Nike leo kiasi amekuwa mchangamfu," amesema Bw Harrison katika video iliyopakiwa kwenye ukurasa wa Facebook wa wakamata nyoka wa Gold Coast na Brisbane .
"[Hata hivyo] ataendelea kulazwa kwa muda mrefu kidogo [katika kitua cha uhifadhi na matibabu ya wanyama cha Currumbin Wildlife Sanctuary] mpaka hali yake itakapotengemaa na kurudishwa mwituni."

Viungo Sita vya Mwili Ambavyo Havihitajiki Tena, na Matumizi Yake ya Awali

Mabadiliko yamejiri baada ya kipindi cha muda mrefu lakini pia ni mchakato wa polepole.
Tabia nyingine zinazidi kusalia katika vizazi vingi hata baada ya kukosa madhumuni.
Vipengele hivi vya uvumbuzi, au sifa za kimwili, hupatikana katika wanadamu pia.
"Mwili wako kimsingi ni makumbusho ya historia ya asili," anasema mwanahistoria wa binadamu Dorsa Amir katika chapisho lake la mtandao wa Twitter.
Kwa nini sifa hizi zinaendelea kusalia hata ingawa zinaonekana kupoteza umuhimu wao? Kwa sababu mabadiliko ni mchakato wa taratibu.
Wakati mwingine, hakuna shinikizo za kutosha dhidi yake, kwa hiyo inasalia kutoka kizazi kimoja hadi chengine.
Katika baadhi ya matukio, hupata kazi mpya katika mchakato wakati vinapofanya kazi mpya.
''Mara nyengine unafikiri labda, je viungo hivi vilitakiwa kutoa huduma gani'', Dorsa Amir aliambia BBC.
Hivi hapa ni viungo hivo sita vilivyowachwa.
1. Mmisuli iliopo chini ya kiganja cha mkono
Kwa mfano weka mkono wako katika eneo lililo tambarare kama meza halafu uguse kidole kidogo hadi kile kikubwa cha mkono wako.
Je unaona misuli karibu na kiganja chako cha mkono ? hiyo ndio inayoitwa Palmaris longus.
Usijali kama huwezi kuona. Takriban asilimia 18 ya watu duniani hawana misuli hiyo na kutokuwepo kwake hakushirikishwi na mapungufu yoyote.
Misuli hiyo hupatikana miongoni mwa sokwe wanaopendelea kupanda miti.
Hii inamaniisha kwamba ilikuwa ikitumika kusaidia kupanda miti.
Siku za hivi karibuni misuli hiyo hupendelewa sana na madaktari wa upasuaji.
''Huitumia mara kwa mara katika upasuaji kwa kuwa haitumiki sana katika kazi za mkono'', alisema Dorsa.
2. Uvimbe mdogo katika sikio.
Viungo Sita vya Mwili Ambavyo Havihitajiki Tena, na Matumizi Yake ya Awali
"Iwapo unaweza kuchezesha sikio lako basi unaonyesha mabadiliko ya binadamu'', anaandika Jerry Coyne katika kitabu chake.
Kwa ni mabadiliko ni ya kweli.
Alikuwa akizungumzia misuli mitatu iliopo nje ya sikio. Uvimbe mdogo uliopo juu ya sikio ni mojawapo ya misuli hiyo.
Miongoni mwa watu wengi, misuli hiyo haina maana yoyote lakini wanaweza kuitumia kuchezesha masikio yao.
Huku ikiwa kuna mjadala wa iwapo msuli huo ulikuwa mkubwa miaka ya mbeleni, inadaiwa kuwa msuli huo katika sikio unaonyesha mabadiliko.
Misuli hiyo hutumika miongoni mwa paka na farasi kuchezesha masikio yao kama inavyoelezwa na Coyne.
Inawasaidia kukabiliana na wanyama wengine, kuwatafuta watoto wao na kuelewa sauti nyengine.
3. Mfupa wa mkia
Viungo Sita vya Mwili Ambavyo Havihitajiki Tena, na Matumizi Yake ya Awali
Mfupa wa mkia bila shaka ni mabaki ya mabadiliko katika binadadamu, kulingana na Dorsa Amir.
Inatukumbusha kwamba tulikuwa na mikia ambayo litumika kusawazisha mwendo wetu katika miti.
Kiungo hicho ni mojawapo ya mifano mizuri ya viungo vinavyofanya kazi nyengine kinyume na ilivyokuwa awali.

4. Kigubiko cha jicho la tatu
Viungo Sita vya Mwili Ambavyo Havihitajiki Tena, na Matumizi Yake ya Awali
Je unaiona sehemu ya rangi ya waridi iliopo katika kona ya jicho lako?
Ni mabaki ya kile kinachojulikana kama utando au "kigubiko cha tatu", kutokana na mabadiliko ya mwanadamu.
Kigubiko cha jicho la tatu husonga kutoka kushoto kwenda kulia, kulingana na Dorsa.
Lakini kwa sasa hakina huduma yoyote katika maisha ya sasa.
Unaweza kukiona miongoni mwa wanyama wengine , kama vile ndege na paka.
5. Msisimko wa mwili bila kutarajia
Viungo Sita vya Mwili Ambavyo Havihitajiki Tena, na Matumizi Yake ya Awali
Je unajua kitendo anachofanya paka wakati anapohatarishiwa maisha yake?
Ni sawa na vile tunavyopata msisimuko wa mwili wakati unaposikia baridi ama hata kuogopa kitu.
Wanasayansi wanakiita kitendo hicho piloerection reflex
Kutokana na vile tunatumia muda wetu mrefu duniani kama wanyama wenye manyoya, msisimuko huo ulikuwa ni mojawapo ya njia za zamani za kukufanya uwe mkubwa zaidi ya ulivyo ama hata kulinda joto kutotoka mwilini wakati unapohisi baridi kulinga na Dorsa
''Wakati tulipoanza kupoteza baadhi ya nywele hizo mwilini , msisimuko huo ulianza kukosa maana hadi kufikia kiwango cha kukosa kazi ya kufanya''.

6. Mshikamano wa mikono

Mshikamano wa mkono unaonekana wakati mtoto anaposhikilia kidole kwa nguvu.
Kitendo hiki hufanyika miongoni mwa wanyama wengine.
''Watoto huzaliwa tayari kuwashika wazazi wao ili kubebwa, inadaiwa kwamba kitendo hicho miongoni mwa wanadamu kilitokana na kitendo hicho'', anaongezea Dorsa.
Lakini watoto wetu hubebwa wakiwa hawajakomaa vya kutosha ikilinganishwa na watoto wa wanyama wengine ambapo hawawezi kuinua vichwa vyao na kutembea.
Hizi ni tabia nyengine ambazo zinatokana na mabadiliko ya mwanadamu. lakini ni mabadiliko ambayo hayamsaidi mwanadamu wa sasa.

Thursday, January 24, 2019

Angalia Hapa Matokeo Ya Kidato Cha Nne Csee 2018 Na Qt 2018 Yametangazwa

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
The CSEE Examinations results for year 2018 have been released by NECTA and below are the Links to help you see the results.
THE NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA (NECTA) is Government Institution which was established by the Parliamentary Act No. 21 of 1973

One STOP For All The Examination Results – New Updates

Saturday, September 15, 2018

Walio na upara sasa wana sababu ya kutabasamu: Dawa ya kutibu upara yapatikana

Walio na upara sasa wana sababu ya kutabasamu: Dawa ya kutibu upara yapatikana
Dawa ya kutibu upara imegunduliwa kwa kutumia dawa ya kutibu mifupa iliodhoofika
Watafiti waligundua kwamba dawa hiyo ina athari kubwa katika mashina ya nywele katika maabara kwa kuzipatia nguvu nywele kumea. Dawa hiyo inashirikisha vipengele vinavyolenga protini ambayo hutumika kukatiza umeaji wa nywele na hivyobasi kusababisha upara.
Kiongozi wa mradi huo Dkt. Nathan Hawkshaw kutoka chuo kikuu cha Manchester alisema inaweza kuleta tofauti kwa watu wanaokabiliwa na ukosefu wa nywele
Ni dawa mbili pekee ambazo hutumika kutibu upara
  • minoxidil, kwa wanaume na wanawake
  • finasteride, kwa wanaume pekee
Dawa zote mbili zina madhara na hukosa kufanya kazi mara nyengine hivyobasi waathiriwa hupendelea kufanya upandikizaji wa nywele badala yake
Utafii huo uliochapishwa katika jarida la PLOS Biology ulifanywa katika maabara, huku sampuli zikiwa na nywele kutoka kwa zaidi ya wagonjwa 40 wa kiume wanaotaka kupandikizwa nywele
Na Dkt. Hawkshaw aliambia SPOTI TV kwamba jaribio litafanywa kuona iwapo tiba hiyo inafanya kazi na ni salama kwa watu
Ni nini kinachosababisha kupotea kwa nywele?
Kupotea kwa nywele ni swala la kila siku na sio tatizo la kukutia wasiwasi. Baadhi ya nywele ni za kudumu huku nyengine zikiwa za muda mfupi.


Presentational grey line

Msemaji wa muungano wa madaktari wa ngozi nchini Uingereza aliambia BBC: Huu ni utafiti muhimu sana
"Watafiti wanasema kuwa kupotea kwa nywele ni tatizo la kawaida na linaweza kuathiri afya yako ikiwemo kukosa kujiheshimu na kujiamini.

TANGAZO LA AJIRA SERIKALINI NA MASHIRIKA BINAFSI LEO, SOMA HAPA👇

''Utafiti zaidi utahitajika kufanywa kabla ya kutumika na watu walio na tatizo la kupoteza nywele''.
Kwa watu wenye tatizo la kupotea kwa nywele, tiba imepatikana.
Hatua hiyo inawapatia waathiriwa afueni kwa kuwa kuna chaguo la dawa ambazo zinaweza kutibu.

Mwanamitindo agongwa na treni akipigwa picha

Mwanamitindo agongwa na treni akipigwa picha
Mwanamke wa umri wa miaka 19, ambaye alikuwa anaanza kujikuza kama mwanamitindo, aligongwa na treni na kufariki alipokuwa anapigwa picha.
Fredzania Thompson alikuwa anapigwa picha hizo zake za mitindo, ambazo zilikuwa za kwanza, kwenye reli alipogongwa na gari moshi.
Picha za Thompson, alizopigwa muda mfupi kabla ya mkasa huo kutokea Navasota, Texas, zimesambazwa na familia yake.
Polisi wanasema alikuwa mjamzito wakati huo na kwamba alikuwa anaondokea treni moja kwenye njia moja ya reli alipojipata ameingia kwenye njia ya reli ambapo kulikuwa na treni nyingine iliyokuwa inapita ambayo ilimgonga.

TANGAZO LA AJIRA SERIKALINI NA MASHIRIKA BINAFSI LEO, SOMA HAPA👇

Gazeti la The Eagle limesema ilikuwa mara yake ya kwanza kwenda kupigwa picha za uanamitindo.
"Bila shaka, hilo jambo alililotaka kulifanya maishani," Hakamie Stevenson alisema kumhusu bintiye.
"Ndiyo shughuli aliyoanza kuifanya siku aliyokumbana na mauti yake."
Polisi wanasema bado wanafanya uchunguzi kuhusu kisa hicho.Afisa wa polisi wa Navasota ameambia SPOTI TV kwamba hata hivyo bado hawajagundua hila yoyote.
Ukurasa umefunguliwa katika mtandao wa GoFundMe kujaribu kuchangisha $10,000 (£8,150) za kugharimia mazishi ya Fredzania.


'Admin' wa WhatsApp afungwa miezi 5 gerezani

'Admin' wa WhatsApp  afungwa miezi 5 gerezani
Mwanafunzi mmoja ametumikia kifungo cha miezi mitano gerezani nchini India kufuatia ujumbe wa Whatsapp ambao anasema hakuutuma.

Taarifa zinasema mwanamume mwenye miaka 21 alishtakiwa kwa uasi kutokana na ujumbe wa 'kutusi', licha ya kwamba haijulikani wazi ujumbe huo unasema nini.
Polisi imemtuhumu mwanamume huyo kuwa msimamizi wa kundi la Whatsapp, wakati malalamiko yalipowasilishwa.
Familia yake inalalamika kwamba aliishia kuwa msimamizi wa kundi hilo baada ya wasimamizi waliokuwepo kulitoroka kundi hilo.
Junaid Khan, mwanafunzi katika mji wa Talen katika jimbo la Madhya Pradesh katikati India alikamatwa mnamo Februari 14. Kwa mujibu wa taarifa katika eneo hilo, mashtaka yanatokana ana ujumbe uliowasilishwa katika kundi hilo la WhatsApp ambalo yeye ni mshirika, na kuchangia yeye kushatkiwa kwa uasi.
Kwa mujibu wa gazeti la The Times of India, Polisi walimkamata Khan kwa kuwa msimamizi wa kundi la WhatsApp wakati kesi hiyo ilipowasilishwa kwao.
Inadhaniwa kwamba mojawapo wa wasimamizi waliokuwepo na kutoroka ndiye aliyetuma ujumbe huo, na inaarifiwa kwamba yeye pia amekamatwa.
Mkuu wa kituo cha polisi cha Rajgarh amelimbia gazeti hilo kwamba wanajaribu 'kuthibitisha iwapo watu wengine pia ni wasimamizi wa kundi hilo pia'.

TANGAZO LA AJIRA SERIKALINI NA MASHIRIKA BINAFSI LEO, SOMA HAPA👇

Umma kuchukua hatua mikononi

Kwa mujibu wa sheria ya mitandao nchini India, wasimamizi wa makundi ya mitandao ya kijamii au admins, wanaweza kufungwa gerezani kwa kusambaza ujumbe unaoonekana kuwa ni tusi kidini au kisiasa.
Huku kukiwa na watumiaji milioni 200 kwa mwezi nchini, mara nyingi watu wengi hukamatwa kutokana na uhalifu katika WhatsApp. Maafisa wanasema hatua zimeidhinishwa kuzuia watumaiji mitandao ya kijamii kuchochea ghasia.
Wiki iliyopita, kampuni hiyo inayomilikiwa na Facebook imetangaza itapunguza kiwango ambacho ujumbe unaweza kusambazwa India, ili kuzuia kusambaa kwa taarifa za uongo katika jukwaa hilo.
Hatua hiyo imetolewa baada ya visa kadhaa vya raia kuchukua hatua mikononi kuhusishwa na ujumbe uliosambazwa katika makundi ya WhatsApp.

WhatsApp: Jambo gani linakukera katika makundi ya WhatsApp uliyopo?

WhatsApp: Jambo gani linakukera katika makundi ya WhatsApp uliyopo?
Makundi ya mitandao ya kijamii ya WhatsApp huwa yanawasilisha umoja wa watu kuwa na malengo yanayofanana.
Lakini hali inakuwa tofauti kwa sababu inaonekana kwamba wengi wanashindwa kufuata kanuni walizojiwekea. Hii inatokea pale ambapo mtu anaingiza maongezi ambayo sio muhimu kwa wakati huo au kuleta ujumbe ambao mahali alipotuma si sahihi.
Je,ni jambo gani ambalo huwa linakukwaza katika makundi ya WhatsApp na namna gani unaweza kuepukana na kero hizo?

TANGAZO LA AJIRA SERIKALINI NA MASHIRIKA BINAFSI LEO, SOMA HAPA👇

Mkuu wa Kundi

Mkuu wa kundi ndio ana mamlaka yote .Hivyo yeye ni muhimu kuweka kanuni zote zitakazoliongoza kundi.
Haitakiwi kuwepo kwa majadiliano baina ya mtu na mtu kwa sababu makundi haya yanajumuisha mawasiliano ya kikundi na sio ya mtu mmoja moja hivyo watu wawili wakiongea masuala yao peke yao kwenye kundi maongezi hayo yanaweza kuwakera wengine.
Kwenye kundi la Whatsapp wana kikundi wanatakiwa kuweka ujumbe ambao unaweza kuwavutia kila mjumbe wa kundi hilo au unaweza kumfurahisha.
Suala la pili ni kwamba suluhisho ni rahisi ili kuepukana na usumbufu ambao unaweza kuwasababishia watu wengine kwa kumuandikia ujumbe binafsi mtu uliyemlenga na sio kwenye kundi.

Hakikisha kwamba unatuma ujumbe sahihi katika kundi sahihi

Unaweza kuhakikisha mara ya kwanza na ya pili na hata mara ya tatu kabla hujabonyeza kitufe cha kutuma ujumbe.
Kwa sababu usipokuwa makini unaweza kujiaibisha na hata kukupelekea kujitoa kwenye kundi na kuwakwepa watu kwa muda ukifikiria aibu uliyoituma katika kundi la whatsapp.

Usiandike maelezo marefu

Andika maneno kwa ufupi isizidi hata sentensi moja au maneno kumi.

Usiwe mjumbe ambaye huchangii mijadala inayoibuka katika kundi.

Katika makundi ya whattsap hakuna nafasi ya watu ambao hawashiriki katika kuchangia maelezo yoyote pale wanapopokea ujumbe na kuusoma bila kujibu
Hii inaleta ugumu pale ambapo wajumbe wengine kwenye kundi wanasubiri majibu kutoka kwa kila mmoja lakini wengine wanakaa kimya.

Muombe idhini mtu kabla ya kumkaribisha katika kundi

Hivi inawezekana kweli kuwakaribisha watu thelathini katika nyumba yako bila kuwafahamu,kiuhalisia jambo hilo haliwezekani,vivyo hivyo na kwenye makundi ya whatsapp ni lazima watu kuulizwa kama atapenda kujumuika kuwa miongoni mwa wana kikundi.
Na vile vile pale unapoondoka katika kundi ni vyema kusema sababu iliyopelekea ufanye uamuzi huo.