Saturday, July 11, 2020

Magazeti ya Leo Jumamosi 11 Julai 2020

Friday, July 10, 2020

Magazeti ya Leo Ijumaa 10 Julai 2020

Full Shangwe mapokezi ya Simba Dar

empty:news-banner-img
Kikosi chetu kikiwa na taji la ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2019/20 kimepokelewa kwa shamra shamra baada ya kurejea jijini Dar es Salaam kutoka mkoani Mtwara. Taji hili tulikabidhiwa jana katika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi baada ya mchezo wetu dhidi ya Namungo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana. Shangwe hizo zimeanzia katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na mpaka makao makuu ya klabu huku idadi kubwa ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakijitokeza barabarani kuilaki. Idadi kubwa ya waendesha boda boda na hawakuwa nyuma walijitokeza kunogesha sherehe hizo ambazo zimefana. Kuanzia saa 3 asubuhi sehemu kubwa ya jiji la Dar es Salaam lilipambwa na rangi nyekundu kutokana na shamra shamra za ubingwa huu ambao tumeutwaa kwa mara ya tatu mfululizo tena tukiwa na mechi sita mkononi.

Thursday, July 9, 2020

PICHA: Matukio mbalimbali ya Shamra Shamra za Ubingwa msimu wa 2019/20

Timu yetu leo imekabidhiwa rasmi taji la ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2019/2020 kwenye sherehe za ubingwa zilizofanyika uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Nahodha John Bocco akiwa ameshikilia kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kukabidhiwa na Waziri Hamis Kingwangala na Rais wa TFF Wallace Karia

Kabla ya sherehe hizo kulitanguliwa na mchezo wa ligi kati yetu na Namungo ambao umemalizika kwa sare ya bila kufungana. Ubingwa huu ni watatu mfululizo kwetu ambapo tuweka rekodi ya kutwaa tukiwa na michezo sita mkononi.
Wachezaji na viongozi wa Simba wakisherehekea baada ya kukabidhiwa kombe la Ligi Kuu ya Vodacom

Nahodha John Bocco akiwa na kombe la ubingwa Ligi Kuu Bara

Wachezaji na viongozi wa Simba wakisherehekea baada ya kukabidhiwa kombe la Ligi Kuu Bara

Nahodha John Bocco na kipa Aishi Manula wakiwa na taji la Ligi Kuu Bara walilokabidhiwa baada ya mechi dhidi ya Namungo FC iliyochezwa Uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa mkoani Lindi

Viongozi wa Simba wakiwa na kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Bara walilokabidhiwa Uwanja wa Majaliwa baada ya mechi dhidi ya Namungo FC

Kutoka kulia ni wachezaji wa Simba, Clatous Chama, Said Ndemla, Hassan Dilunga na Aishi Manula wakiwa na kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Bara walilokabidhiwa Uwanja wa Majaliwa baada ya mechi dhidi ya Namungo FC

Simba yananyua ndoo kwa sare mbele ya Namungo

Mchezo wa ligi dhidi ya Namungo ambao umetumika kwa kukabidhiwa taji la ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2019/2020 uliopigwa uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi umemalizika kwa sare ya bila kufungana. Katika mchezo wa leo kocha mkuu Sven Vandenbroeck amewatumia wachezaji wengi ambao walikosa nafasi katika mechi kadhaa zilizopita. Kwenye mtanange huo ambao ulikuwa mkali timu zote zilitengeneza nafasi kadhaa za kufunga huku zikishambuliana kwa zamu lakini hakuna aliyeweza kupata bao. Mchezo huu ni wapili mfululizo wa ligi kwa kutoka sare ya bila kufungana baada ya ule uliopita dhidi ya Tanzania Prisons uliopigwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Baada ya shamra shamra za ubingwa kikosi kitarejea mkoani Mtwara na kesho kitapaa hadi jijini Dar es Salaam tayari kwa maandalizi ya mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya siku ya Jumapili.

Magazeti ya Leo Alhamis 9 Julai 2020