Sunday, June 21, 2020

Sven aijia kivingine Mwadui, Fraga, Ndemla, Kennedy wote ndani

Tags

empty:news-banner-img

Sven aijia kivingine Mwadui, Fraga, Ndemla, Kennedy wote ndani

Kocha mkuu, Sven Vandenbroeck kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Mwadui FC amepanga kikosi tofauti na ilivyozoeleka ikiwa ni njia ya kuhakikisha anabaki na pointi zote tatu nyumbani. Katika mchezo wa leo ameanzisha mabeki watatu wa kati kitu ambacho sio kawaida kukifanya ambapo amewaanzisha kwa pamoja Kennedy Juma, Pascal Wawa na Erasto Nyoni. Mara nyingi kocha Sven amekuwa akitumia mabeki wawili wa kati ambao ni Wawa na Erasto au wakati mwingine Tairone Do Santos na Kennedy lakini leo kawaanzisha watatu. Katika idara ya ulinzi wa kukaba kawaanzisha kwa pamoja Gerson Fraga na Said Ndemla ambapo mchezo uliopita alimtumia Mzamiru Yassin katika eneo hilo kufuatia Jonas Mkude kuwa majeruhi. Sven pia amefanya mabadiliko kwenye idara ya ushambuliaji leo tutaongozwa na nahodha John Bocco akisaidiwa na Luis Miquissone na Hassan Dilunga wakati kinara Medie Kagere ambaye mara nyingi huanza lakini leo atatokea benchi. Kikosi Kamili kitakachoshuka dimbani: 1. Aishi Manula 2. Shomari Kapombe 3. Mohamed Hussein 4. Kennedy Juma 5. Pascal Wawa 6. Erasto Nyoni 7. Gerson Fraga 8. Said Juma 9. John Bocco © 10. Luis Miquissone 11. Hassan Dilunga Wachezaji wa Akiba Gk. Ally Salim 2. Yusuf Mlipili 3. Mzamiru Yassin 4. Clatous Chama 5. Medie Kagere 6. Francis Kahata 7. Shiza Ramadhan