Sunday, June 21, 2020

Mechi ya kisasi... Kocha, wachezaji wafunguka

Tags

empty:news-banner-img

Mechi ya kisasi... Kocha, wachezaji wafunguka

Saa chache zimebaki kabla ya mchezo wetu wa pili wa ligi ambao utakuwa dhidi ya Mwadui FC, mchezo unaotabiriwa wa kisasi kutokana na matokeo ya mzunguko wa kwanza wa kwanza wa ligi ambapo tulipoteza mchezo huo.
Mechi hiyo itakayopigwa katika Uwanja wa Taifa ambapo Simba inaenda ikiwa na kumbukumbu ya Oktoba 30 mwaka jana ilipopoteza mchezo huo katika Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga kwa bao moja ikiwa mechi ya kwanza kupoteza kwenye ligi. Mapema wiki hii Kicha Mkuu, Sven Vandenbroeck ameweka wazi kuwa mchezo wa leo utakuwa mgumu na wanaiheshimu Mwadui lakini lengo kuu ni kuhakikisha pointi zote tatu zunabebwa na Simba. "Mchezo utakuwa mgumu, Mwadui ni timu bora na ilitufunga mzunguko wa kwanza lakini tumejipanga kuhakikisha tunalipa kisasi. Wachezaji wote wapo katika hali nzuri tayari kwa mchezo," amesema Kocha Sven. Kwa upande wake Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu amesema maandalizi yote yamekamilika na wachezaji wawili wataukosa mchezo huo ambao ni Jonas Mkude ambaye ni majeruhi na Sharaf Shiboub aliye Sudan ambapo akisubiri mipaka ya nchi hiyo ifunguliwr kutokana na mlipuko wa virusi vya corona. Kwa upande wake mlinzi wa kati Erasto Nyoni amesema morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja anataka kuhakikisha ushindi unapatikana na watapambana kulifanikisha hilo. "Sisi kama wachezaji tupo kamili na tayari kwa ajili ya mchezo wa leo, tumejiandaa vizuri na makocha wetu wameyaona mapungufu ya mchezo uliopita wameyafanyia kazi tunaamini tutapata ushindi leo," amesema Erasto. Naye mlinda mlango namba moja, Aishi Manula amesema kwa sasa kila mchezaji lengo lake ni kuhakikisha tunatetea taji la ligi na kushinda mechi zote tisa zilizobaki. Matokeo ya mechi nne zilizopita kati yetu na Mwadui Mwadui 1 -0 Simba Simba 3 -0 Mwadui Mwadui 2-2 Simba Mwadui 1-3 Simba