Zidane apambana na Pogba

Zidane apambana na Pogba
Zidane apambana na Pogba
LONDON, ENGLAND.KOCHA wa Real Madrid Zenedine Zidane hajaachana na Paul Pogba, bado anamsaka. Anataka kuharakisha kumsajili kabla ya dirisha la usjaili la Ulaya halijafungwa.

Manchester United haikusajili kiungo mpaka dirisha la usajili la Ligi Kuu England lilipofungwa jana lakini sasa wanatakiwa kuendelea kupambana na Real Madrid ambayo inamsaka mchezaji huyo huku ikizingatiwa kwamba dirisha la usajili Ulaya linafungwa Septemba 2.

Habari njema ni kwamba Bosi wa Real Madrid Florentino Perez yupo tayari kutumia kiasi kisichopungua Pauni 200 milioni kwa ajili ya kusajili mchezaji mwenye hadhi.