Zarinah Aibu Tena Uganda

Zarinah Aibu Tena Uganda
BADO mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ anazidi kuandamwa vibaya nchini kwao, Uganda, baada ya kupigwa chini kuwa jaji katika Shindano la Miss Uganda, jambo lililotafsiriwa ni aibu nyingine kwake. Hatua hiyo inakuja baada ya Zari ambaye ni raia wa Uganda anayeishi nchini Afrika Kusini kwa sasa, kutibuana ukumbini na MC wa shughuli hiyo, Anita Fabiola wakati wa shindano hilo kwa mwaka 2019 ndani ya Sheraton Hotel jijini Kampala, Uganda hivi karibuni.

Kwa mujibu wa habari kutoka Kampala, uongozi wa shindano hilo umefikia uamuzi wa kufanya mabadiliko kwa kumuondoa Zari kwa kile kilichodaiwa alilitia aibu shindano hilo. “Mabadiliko hayo yamekuja kutokana na drama zilizoshuhudiwa ukumbini siku ya fainali kati ya Zari na Anita.

“Lakini mwathirika mkubwa wa mabadiliko haya ni Zari kwa sababu yeye ndiye ameondolewa kwenye ujaji ambao amekuwa akiushikilia kwa miaka kadhaa,” ilisomeka sehemu ya habari hiyo mbaya juu ya Zari ambaye ni mzazi mwenzake wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye amezaa naye watoto wawili, Tiffah na Nillan, kabla ya kutengana.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uganda, Zari anatuhumiwa kumkosea heshima Anita, jambo lililoibua ukosoaji kutoka kila kona na kusababisha kuharibu sifa za shindano hilo kubwa nchini humo.

Hata hivyo, awali uongozi wa Miss Uganda haukutaka kusema chochote, lakini wikiendi iliyopita ulivunja ukimya kupitia kwa mkurugenzi mtendaji wake, Brenda Nyanyonjo.

Kwa upande wake Brenda alithibitisha Zari kupigwa chini kuwa mmoja wa majaji wa shindano hilo. Brenda alisema: “Miss Uganda tunalaumiwa kwa kuonesha tabia au roho mbaya, lakini hilo siyo tunalolisimamia, wavurugaji tumeshawatupilia mbali.”

Ugomvi wa Zari na Anita unatajwa kuwa na mizizi ya muda mrefu huku Diamond au Mondi akihusishwa. Kuna madai yasiyo rasmi kwamba, Zari alishamtuhumu Anita kuchepuka na Mondi siku za nyuma, kidonda ambacho bado hakijapona hivyo shindano hilo lilisababisha kutoneshwa pale Anita