Zari Hassan Afunguka Kuhusu TETESI za Kumcheat Diamond

Zari Hassan Afunguka Kuhusu TETESI za Kumcheat Diamond
Mzazi mwenza wa Daimond Platnumz Zarina Hassan ‘Zari The Boss lady’ amesema hajawahi kutembea na mwanaume yeyote mwingine wakati yuko kwenye uhusiano na mwanamuziki huyo.

Katika mahojiano yake na mtandao wa Millard Ayo, Zari amesema tuhuma zilizotolewa na Diamond kuwa alitembea na moja ya wasanii mapacha kutoka P Square na aliyekuwa mkufunzi wake wa gym wakati yuko kwenye uhusiano na msanii huyo si za kweli.

“P Square ndiyo alikuwa wa kwanza kumwambia Diamond tusiachane kwa sababu familia ni kitu bora kuliko chochote. Tulikuwa tunaingia karibu miaka minne, kwaajili ya maisha yangu, ya wanangu, nilikubali kupoteza kila kitu ikiwemo nafsi yangu kwaajili yake, Mungu ndiyo shahidi wangu. Sijawahi kutembea na mwanaume yeyote yule,” Zari amesema.

“Nilizama katika penzi lake, na kwa sababu nilihisi kwamba nimetoka katika uhusiano mwingine, kwa hiyo nilitaka pia kuujenga uhusiano wangu uwe imara kama uliopita, na nilidhani hata ungekuwa ni wa milele, sijawahi kumdanganya Diamond.”Amesema Diamond alikuwa anatafuta sababu ya kuvunja uhuiano wao kwa sababu tayari alikuwa anajua amefanya kosa la kupata mtoto mwingine nje ya uhusiano wao, hali iliyosababisha kuongea maneno mengi ya uongo.
MaoniMaoni Yako