ZAHERA AUNGURUMA KUFUATIA TETESI ZA KUTIMULIWA YANGA SC


Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera ameshangazwa na tetesi za kuwa anataka kufutwa kazi ndani ya klabu hiyo yenye masikani yake mitaa ya Twiga na Jangwani . 

Zahera amesema hahofii lolote kwani anajua kila kocha anayeajiriwa muda wowote anaweza kufukuzwa kazi.

Sambamba na hilo, Zahera ameweka habari hizo zinamfanya ashindwe kufanya kazi yake kwa ufasaha kwa kukosa utulivu wa kuhojiwa mara kwa mara pia kisaikolojia zinaondoa imani kwa wachezaji na wanachama kuithamini kazi yake . 

Zahera amesema ana ofa tano mezani hata leo akiamua kuondoka Yanga anachangua ni wapi ataelekea. Zahera ametaja mpaka sasa ana ofa kutoka timu za Stade Rennais FC na Stade de Reims zinazoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa (Ligue 1), Motema Mapembe na AC Rangers zote za DR Congo na Kanno Pilars ya Nigeria. 

" napambana na hizi tetesi ili niweze kuivusha timu hatua hii ya klabu bingwa pia kuanza vyema msimu wa ligi kuu lakini pia hata kama nitaondoka, lazima niweke misingi yakuanzia kwa kocha ajaye ili Yang iwe imara kama wote tulivyokubaliana kwenye vikao mbalimbali "
MaoniMaoni Yako