Zahera aligundua tatizo Yanga aahidi kuwaua Township kwao


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa bado kikosi chake hakijawa na maelewano mazuri jambo ambalo liliwapa taabu kupata matokeo kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Township Rollers.

Yanga jana imelazimisha sare dhidi ya Township Rollers, mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa kwa kufungana bao 1-1.

Mchezo wa marudiano wa kimataifa unatarajiwa kuchezwa  kati ya Agosti 23-25 nchini Botswana.

"Wachezaji wangu bado wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kuelewana wakiwa ndani ya uwanja jambo ambalo linaleta ugumu kwenye kupata matokeo uwanjani.

"Kwa sasa hesabu ni kuona kwamba tunakuwa na kikosi imara ambacho kitapata matokeo kwenye mchezo wetu wa marudio, mashabiki waendelee kutupa sapoti katika hili, nami nitafanyia kazi makosa yote," amesema.
MaoniMaoni Yako