Saturday, August 17, 2019

Zahera aanza nyodo Yanga

Tags

Zahera aanza nyodo Yanga
Wakati huohuo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameahidi kuwa na msimu mzuri huku akitamba kuchukua kila kombe watakalolishindania likiwemo la Ligi Kuu Bara.

Ametoa kauli hiyo wakati wakiwa kwenye Chuo cha Mwika Wildlife maeneo ya Moshi mkoani Kilimanjaro ambako wameweka kambi kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

“Nimefanya maboresho makubwa ya kikosi changu hali inayonipa matumaini ya kuchukua kila ubingwa tutakaoushindania katika msimu huu na hilo linawezekana kwangu.

“Nataka msimu huu kuchukua ubingwa wa ligi na Kombe la FA mfululizo na kufika mbali katika Ligi ya Mabingwa Afrika, tutaanza kwa kuwaondoa Township ili tusonge mbele zaidi,” alisema Zahera.

Ikumbukwe kuwa, msimu uliopita Yanga ilimaliza ligi kuu ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Simba iliyotwaa ubingwa, pia iliishia Hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la FA.