Saturday, August 3, 2019

Yanga Yazindua Jezi Zao Mpya

Tags

   Yanga Yazindua Jezi Zao Mpya

KLABU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam,  leo imetambulisha jezi zake kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano ya ndani na kimataifa ambazo zimetengezwa na kampuni ya GSM ya Dar es Salaam.

Jezi hizo zimezinduliwa katika Hotel ya  Serena, Dar es Salaam,  ambapo zile za rangi ya kijani zitakuwa za nyumbani na zile njano zitakuwa ni za ugenini.


Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba (wa pili kushoto) akikabishiwa jezi na Msolla.Mtendaji mkuu wa GSM, Eng. Heris Said, amesema kwa mara ya kwanza Tanzania kumezinduliwa jezi bora ambazo hazijawahi kutokea na akawaasa mashabiki wa  Yanga kununua jezi halisi.Yanga itaanza kuzitumia jezi hizo keshokutwa Jumapili katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Kariobangi Sharks kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi.