Yanga yawahukru Mashabiki Baada Ya Kuhitimisha Wiki Ya Mwananchi

Yanga yawahukru Mashabiki Baada Ya Kuhitimisha Wiki Ya Mwananchi
FREDRICK Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa mashabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga wanahitaji pongezi na shukrani kwa kujitoa kwa hali na mali siku ya jana.

Yanga jana ilihitimisha kilele cha Wiki ya Mwananchi uwanja wa Taifa ambapo walicheza mchezo wa kirafiki na Kariobangi Sharks na kutambulisha jezi mpya pamoja na wachezaji wake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mwakalebela amesema kuwa ni jambo la kihistoria kwa wanachama wa Yanga pamoja na mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa.

"Tuna kila sababu za kuwashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa na ni historia imewekwa kwa kweli hivyo shukrani kwa mashabiki na ni mwanzo mzuri kwetu.

"Tulianza wiki kwa kufanya mambo ya kijamii ambapo tulitembelea hospitali, kufanya usafi, kukarabati baadhi ya miundombinu pamoja na kutembelea watoto yatima hivyo tunapaswa kuendelea na moyo huo," amesema.
MaoniMaoni Yako