Saturday, August 17, 2019

Yanga Yatuma Ujumbe Mzito Kwa Township Rollers

Tags


JUMA Abdul, beki wa Yanga amesema kuwa kwa namna kikosi cha Yanga kilivyo wana imani ya kwenda kupata matokeo mbele ya Township Rollers kwenye mchezo wa marudio.


Abdul na Yanga wamefikia makubaliano mazuri na amejiunga na kikosi kilichoweka kambi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kuiwinda Rollers na jana alikuwa kwenye kikosi kilichopoteza mbele ya Polisi Tanzania.

Ujumbe huo ni maalumu kwa wapinzani wao Rollers ambao watarudiana nao Agost 24 nchini Botswana kwenye mchezo wa awali Ligi ya Mabingwa Afrika.


Akizungumza na Saleh Jembe, Abdul amesema kuwa kikosi kipo imara na kina wachezaji wengi wazuri hivyo mashabiki wasiwe na mashaka katika hilo.


“Tunajua kwamba kwa sasa tuna mchezo mgumu wa marudio na mashabiki wengi wanatutazama ni namna gani tutafanya, hilo halina mashaka kazi itafanyika kwani wachezaji wote wana morali.


“Nimerejea rasmi na kazi itaonekana uwanjani kwani mpira kwangu ni kipaji na nina uzoefu na mechi za kimataifa kwa ushirikiano na wachezaji tutafanya kitu kizuri,” amesema.