Sunday, August 18, 2019

Yanga Yaitandika AFC Leopards Huko Arusha, Zahera Asema Walienda Kupoteza Muda..

TagsMchezo wa kirafiki wa kimataifa uliowashirikisha mabinwa wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania, Yang SC umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi mwembamba wa goli 1 - 0 dahidi AFC Leopards.

Alikua ni nahodha, Papy Tshishimbi aliyewaamusha Wananchi waliofurika katika dimba la Shekhe Amri Abeid kwa kuzamisha kimiani mpira wa kona uliopigwa na Patrick Sibomana mnamo dakika 83' na kuwaweka Wananchi kifua mbele.

Mara baada ya mchezo huo kumalizika kocha mkuu wa klabu hiyo Mkongomani Mwinyi Zahera atupia lawama zake kwa waandaaji wa michezo yote ya kirafiki ambayo timu yake imeicheza huku lawama kubwa zikiwa juu ya viwanja huku akisema kambi yake ya Arusha na Kilimanjaro ni kupoteza Muda.

"Tuna mchezo mgumu na muhimu wa marudiano dhidi ya Township Rollers, nahitaji muda kuiandaa timu lakini tunakuja kupoteza muda huku Moshi na Arusha. . tunacheza na Polisi kisha AFC katika viwanja vibovu hakuna jambo la maana tulilofaidika nalo hii ziara tungeweza kuifanya muda mwingine sio huu. . jambo la msingi nna matumaini ya kwenda kufanya vema kule Botswana kwa maana tutacheza katika uwanja mzuri" 
-Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Zahera Mwinyi.