Yanga Waiangukia Bodi Ya Ligi..Uongozi wa Yanga umewasilisha barua Tff kuiomba bodi ya ligi isogeze mbele mechi yao ya kwanza ya ligi kuu Tanzania bara.

Makamu mwenyekiti wa kamati ya Mashindano Saad Kimji amesema kwamba sababu ya kuomba mchezo huo kusogezwa mbele ni kutokana na kubanwa na ratiba ya ushiriki wa mechi yao ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Township Rollers ya nchini Botswana.

Kimji amesema kikosi cha timu hiyo kitacheza mchezo huo ugenini tarehe 24 na tarehe 26 kuamkia 27 timu itaanza safari ya kurejea hapa nchini,hivyo kucheza mechi yao ya Ligi tarehe 28 ni jambo ambalo anaamini halitawezekana.

Amesema kwamba lengo Lao ni kuiomba bodi ya ligi ili mechi hiyo iliyopangwa kuchezwa tarehe 28 sasa ichezwe tarehe 30 mwezi huu ili timu ipate muda wa kupumzika.
MaoniMaoni Yako