Yanga Uso Kwa Uso Na Lwandamina CAF Champions LeagueMara baada ya Yanga kuwaondosha Township Rollers katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika sasa Yanga itakutana na Zesco United ya Zambia inayonolewa na kocha wa zamani wa klabu hiyo George Lwandamina na kiungo fundi aliyewahi kukipiga jangwani Thaban Kamusoko kwenye chezo wa raundi ya kwanza ya klabu bingwa Afrika (Caf Champions League).

Mchezo wa mkondo wa kwanza Utapigwa  Dar es salaam na mchezo wa marudiano Zambia. Yanga ikifuzu hapa Inafuzu Makundi ya klabu bingwa Afrika (Caf Champions League) na ikitolewa itaenda kucheza hatua ya Mtoano wa kufuzu Makundi ya Caf Confederation Cup.
MaoniMaoni Yako