Tuesday, August 13, 2019

Yanga, Dante kukaa mezani kuyamaliza

Tags

Yanga, Dante kukaa mezani kuyamaliza

Dar es Salaam. Viongozi wa Yanga wanatarajia kumalizana leo na beki wa kati Andrew Vicent 'Dante' aliyekuwa kwenye mgomo akishindikiza kulipwa stahiki zake na klabu hiyo.

Akizungumzia suala la Dante makamu mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema leo wanaweza kumalizana naye.

"Tumewasiliana naye nadhani suala lake litaisha na ndani ya siku hizi mbili tatu ataunga na wachezaji wenzake mkoani Kilimanjaro," alisema Mwakalebela.

Wachezaji wengine ambao nao walikuwa wakidaiwa kugoma ni Juma Abdul na Kelvin Yondani ambao wamemalizana na klabu hiyo.

Yondani na Abdul ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao wapo kwenye msafara wa kwenda Kilimanjaro kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers.