Sunday, August 18, 2019

Welbeck Atuma Ujumbe Huu Kwa Arsenal

TagsStraika wa zamani wa zamani wa klabu ya Arsenal, Danny Welbeck ametoa shukurani zake za dhati kwa klabu hiyo ambayo ameitumikia kwa kipindi cha miaka mitano akitanabaisha kua alionyeshwa upendo wa kipekee.

Aidha amepeleka shukurani zake pia kwa wapenzi na mashabiki wa washika mitutu hao wa Jiji la London, Arsenal na kusema kuwa hawezi kuusahau ushirikiano waliompatia katika kipindi chote alichua nao.

Straika huyo ambaye amewahi kukipiga kunako vilabu tofautitofauti vikiwemo Preston na Manchester United kwa sasa amejiunga na klabu ya Watford akitokea Arsenal..


Image