Monday, August 19, 2019

Watatu Yanga Kuwakosa Township Rollers

TagsSasa rasmi golikipa namba moja wa klabu ya Yanga, Farouk Shikalo, Beki Mustapha Selemani na Mshambuliaji David Molinga Ndama Falcao wataikosa mechi ya marudiano ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana mchezo ambao utachezwa jumamosi ya August 24.

Sababu kubwa ni kuchelewa kupata Leseni zao kutoka CAF ni hii imetokana na klabu ya Yanga kuchelewa kutuma ITC zao CAF. Sio Yanga tu hata KMC nayo inawakosa baadhi ya wachezaji wake wapya na CAF imesema wachezaji hao wataruhusiwa kucheza kuanzia michezo ya raundi ya kwanza.