Friday, August 16, 2019

Wadada Mjue Hili Swali la “Utakuja Lini Kwetu Kujitambulisha?” Linavunja Mahusiano Mengi Sana

Tags

Wadada Mjue Hili Swali la “Utakuja Lini Kwetu Kujitambulisha?” Linavunja Mahusiano Mengi Sana

Tatizo kubwa la wadada wakisgafikisha miaka 28 kuendelea, ukimtongoza anafikiri kuwa unataka kumuoa, mara ghafla anaanza kukupa mipango ya miaka kumi ijayo mpaka unaanza kuboreka. Mtu hata miezi mitatu hamjamaliza ashaanza kukuuliza “Kwetu unakuja lini?” Dada zangu nije kufanya nini? Kwamba kuna staili ambazo huwezi kunipa mpaka nije kwenu? Hapa ndipo wadada wengi wanaanza kuboa, kwakua ukimuambia kuwa nikama wanalazimishia ukajitambulishe wakati wewe unataka kustarehe.

Nafasi za Kazi Bonyeza HAPA

Maswali yanakua mengi, visirani vinakua vingi mpaka mwanaume unaanza kuwaza “Hivi kama miezi mitatu hivi ananuna mpaka mdomo unanuka kisa tu sijapokea simu yake nitaweza kuishi naye mpaka afe huyu?” Dada zangu mimi nawalewa, lakini unaja wako umekula huko na X wako, mmekaa miaka 7 unampikia na kumpakulia hajaja hata kwenu kuangalia TV, mimi nimejuana na wewe miezi mitatu unataka nikajitambulishe?

Unataka mwanaume akajitambulishe kwenu, mtu hata X wake hajaachana naye vizuri, mwingine alichawa anasubiri akama ataerudiwa au la unataka akajitambulishe kwenu halafu? Najua umri umeenda lakini punguza kasi, tena mwanamke unatakiwa kushtuka umekaa na mwanaume miezi mitatu anataka kuja kwenu kujitambulisha, narudia unatakiwa kushtuka kwani mara nyingi wa namna hiyo naye ni kichomi tu hivyo chunguza kidogo.

Hili swali la “Utakuja lini kwetu kujitambulisha?” Linavunja mahusiano mengi sana, wanawake wanakua na wasiwasi sana wa kuachwa mwanaume akishindwa kulijibu, kibaya Zaidi nikuwa mwanamke anakua na maswali mengi, wasiwasi ambao unageuka na kuwa kisirani, kwa namna hiyo mwanaume anakuchoka, hata kama una mzuka wa kuolewa acha kuuliza kwanza hembu msome mwanaume na si kukimbilia kuuliza wakati unaona matendo yake hayaelekei!

Nafasi za Kazi Bonyeza HAPA