Saturday, August 17, 2019

Vodacom warejea Ligi Kuu Bara kwa masharti

Tags

Imeelezwa kuwa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom imekubali kudhamini tena Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao.

Vodacom ambao awali walijiondoa baada ya kutokuwa na maelewano baina yao na Bodi ya Ligi wamekubali kuweka kitita cha shilingi za kitanzania bilioni tatu.

Fedha hizo zinawekwa kwa masharti wakitaka timu nne zipungue kutoka 20 mpaka 16 ili kuendana na matakwa yao wanayoyataka,

Ikumbukwe katika misimu miwili iliyopita timu za Ligi Kuu ziliongezeka na kufikia 20 maamuzi ambayo yamechukua muda mrefu zaidi kufanyika.

Kuna uwezekano wadhamini hawa wakatangazwa leo katika mchezo wa Ngao ya Jamii baina ya Simba na Azam ama siku yoyote kuanzia leo.