Monday, August 5, 2019

VIDEO: Huku Bunju kumenoga

Tags

MASHABIKI wa klabu ya Simba wamefika uwanja wa Bunju ambao unamilikiwa  na klabu hiyo huku wakionyesha kurudhishwa na maendeleo ya ujenzi wa uwanja wao.
Ni zaidi ya miaka mitano uwanja wa Simba unakuwa kwenye hadithi za ujenzi lakinj sasa uongozi chini ya Mwenyekiti wao wa Bodi ya Wakurugenzi unaonyesha kuweka nia ya dhati ya kuujenga.
Simba sasa imeamua kujenga viesnja viwili kwa mpigo ambapo kimoja kitakuwa cha mazoezi na mwingine kwa ajili ya mechi z amashindano.
Awali uongozi wa Simba ulipanga kujenga uwanja mmoja wa mazoezi ambao ulitakiwa kukabidhiwa mapema mwaka huu lakini baadaye uongozi ulibadilisha mawazo na kuamua kujenga viwanja viwili.
Mashabiki wakionekana wenye nyuso za furaha huku wakiwa wanacheza ngoma zilizokuwa zikipigwa na matawi yao yaliyofika hapa.
Leo Jumatatu, Simba wanaweka jiwe la msingi ambalo linatarajiwa kuwekwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamadunj na Michezo  Dk Harison Mwakyembe.