Monday, August 19, 2019

USM Alger yatembeza bakuli

Tags

USM Alger yatembeza bakuli

USM ALGER inayoshiriki ligi kuu nchini ALGERIA na mashindano ya kimataifa barani africa CAF imekumbwa na ukata wa pesa na kushindwa kulipa mishahara ya wachezaji tangu mwezi wa 3.

Vile vile klabu imeshindwa kulipa ada ya usajili kwa wachezaji wapya msimu huu huku menejiment ya klabu hiyo ikijitahidi kutatua jambo hilo la ukata kutoka kwa wadau mbalimbali na taarfa za ndani zinadai kuwa kuna uwezekano kujitoa mashindano ya CAF msimu huu endapo haili itaendelea hivi hivi hata kama watafuzu hatua ya makundi .

Klabu pia ilikuwa kwenye hati hati ya kukosa nauli na mahitaji muhimu kuifuata CS CASSABLANCA kwa ajili ya mpambano ila wadau na wapenzi wa klabu hyo wamejichanga na kufanikisha kupatikana kwa fedha zitakazoiwezesha klabu hiyo kukidhi taratibu nzima kwa ajili ya mchezo huo.

Haya ni mapito na magumu yoyote yanaweza mtokea tuungane tusitofautiane na kuweka makundi hii ni klabu yetu sote" maneno ya mkurugenzi klabu hiyo HOSSAM