Mambo ya kufanya baada ya kuachwa katika mahusiano ya kimapenzi

Mambo ya kufanya baada ya kuachwa katika mahusiano ya kimapenzi
Mambo ya kufanya baada ya kuachwa katika mahusiano ya kimapenzi
Kuvunjika moyo ni moja ya jambo zito na ambalo mtu hupitia na inahitaji sana moyo kwa sababu ya kupitia wakati mgumu, fikra, mawazo, maumivu, kujiona huna thamani, jamani mtu kaamua kukuacha wa nini kumganda.

Yafuatayo ndiyo mambo muhimu unayopaswa kujifunza pale unapokuwa umeachwa;

Jifunze kuacha yapite.
Muache aende kama alivotaka, duniani hayuko peke yake, mbona wamejaa kama yeye na unaweza kupata mzuri zaidi yake na ufurahie sana na kumshukuru Mungu.

Usikae peke yako kipindi hiki
Jaribu kukaa na familia, marafiki na watu wako wa karibu, cheka, furahia kile unachokifanya yako. Hii ni moja ya safari ya kuanza kumsahau.

Usiwaze kwamba wewe ndio sababu
Kama kuachana mmeshaachana, kwa nini ujilaumu? Mara nyingi mtu unayempenda akikuacha, kuna hali ya kibinadamu inakuja na unajikuta kama unatafuta mapungufu yako ili uweze kujilaumu.

Hii haiwezi kukusaidia. hebu fikiria hata kama wewe ndio umesabababisha kuachana kwenu, je ukishajilaumu ndio utakua umerudisha wakati nyuma ili mapenzi yenu yandelee kuwa moto moto?

Usifanye maamuzi yasiyo na mpango
Mara nyingi watu hukasirika na kwend kufanya sex hovyo hovyo pindi wanapotendwa au kuachwa na watu wanaowapenda. Hebu fikiria hapo anayeumia ni nani?

Utaenda kufanya sex na mtu mwingine kwa lengo la kulipiza kisasi kwa mtu ambaye hana mpango na wewe? Jitahidi sana kuepuka makundi ya watu ambao wanaweza kukuingiza kwenye mtego huu.

Tafuta njia nyingine ya kutoa mawazo na kukupungizia stress. Jitahidi kufanya vitu il uwe na furaha na sio depression ukaja kufa bure siku sio zako ndugu.

Wekeza kwenye furaha yako
Wataalamu wanasema mazoezi ni dawa ya vitu vingi sana mwilini. Jikite katika mazoezi mfano kukimbia au jiweke busy na kazi yoyote ili kukuweka busy na kupoteza attention katika kichwa ya yule aliekuumiza, usijiumize kabisa.

Unajiona maumivu yanazidi, zidisha kujiweka busy na jiweke kama hujawahi kuumizwa na jipe moyo be you as you, duniani hayuko peke yake.

Lenga kwenye mazuri yako
Badala ya kuangalia mabaya ya kuvunjika uhusiano, wewe tizama yale mazuri tu uloyafanya, siku hizi  unaweza kutendwa kweupee na huna kosa ulilolifanya, unajishangaa unakaushiwa tu,usijitie mnyororo wa roho buree ukasema hata nkitongoza naweza nisikae nae sana kama wa mwanzo.

Wanaume wameumbiwa wanawake na wanawake wameumbiwa wanaume, so hata ukiumizwa haifai kusema sitopenda tena, ohh sijui sitokuja kutafuta mwenza tena, inamaana utaweza kukaa ivo pekeako mpaka uzeeni mpaka kufa.

Ni rahisi watu kuvutiwa na wewe endapo utakua unaonesha kama maisha unayamudu.
MaoniMaoni Yako