Yanga Yaanza Ligi Kwa Kupapaswa Na Ruvu Shooting

Tokeo la picha la yanga vs ruvu shooting 0-1


Timu ya soka ya Yanga imeianza vibaya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kwa kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Mchezo huo wa kwanza wa ligi msimu huu kwa timu zote mbili, Yanga licha ya kumiliki zaidi mpira wamejikuta wakiruhusu bao pekee dakika ya 21 kupitia kwa Sadat Mohamed akimalizia pasi ya Said Dilunga. Mara baada ya mchezo huo, Msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire amezidi kutamaba akisema kikosi cha timu yake mwaka huu ni bora kuliko vikosi vyote alivyowahi kuviona hivyo endapo sharia za soka zitafuatwa, basi timu hiyo ndiyo itakayochukua ubingwa wa ligi msimu huu. Masau amesema aliingia kwenye mchezo huo akijua matokeo kwa kuwa alikuwa akiwaamini zaidi wachezaji wa kikosi chake licha ya kuwa ni vijana wa kitanzania na ametamba kuendelea kuwapapasa wengine atakaokutana nao msimu huu.
MaoniMaoni Yako