Tetesi za soka Ulaya leo Jumapili 04.08.2019: Coutinho, Sane, Pogba, Fernandes, Neres, Van de Beek, Neymar

Arsenal wanatarajiwa kuanzisha mazungumzo na Barcelona kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Phillipe Coutinho 27 hatua ambayo itaigharimu klabu hiyo dau la £27m. (Sun on Sunday)
Manchester United wamewasilisha ombi la dau la £46m kumsajili mchezaji wa Ajax mwenye umri wa miaka 22 na raia wa Brazil David Neres. (Yahoo - in Portuguese)
Mchezaji wa Ufaramnsa na Manchester United Paul Pogba anahofia huenda akashindwa kuelekea Real Madrid huku mabingwa hao wa Uhispania wakikabiliwa na dau la £270m kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Manchester United. (Sunday Mirror)
Bayern Munich wanakaribia kumsajili winga wa Manchester City raia wa Ujerumani Leroy Sane baada ya kukubali kandarasi na masharti na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Sky Sport Germany - in German)
Sane anakabiliwa na uwezekano wa kupoteza £11m katika mshahara wake iwapo ataendelea kukataa kutia kandarasi mpya na Man City . (Sunday Mirror)
Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anapima uwezekano wa kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid Isco na beki wa Bournemouth Nathan Ake, 24. (Sunday Express)
Manchester United wamefanya mazungumzo ya kubadilishana wachezaji na Juventus ambapo mchezaji wa Argentina Paulo Dybala, 25, na mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic wataelekea Old Trafford, huku naye mchezaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, akielekea Juventus. (Sunday Times - subscription required)
Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anataka kumsaini beki wa zamani wa Uingereza Gary Cahill, 33 kwa mkopo wa miaka miwili. (Sun on Sunday)
Barcelona inajiandaa kuanza mazungumzo na PSG kuhusu kumununua mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, back to La Liga. (Goal.com)
Kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 24, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho wa manchester United ameambia klabu ya Sporting Lisbon kwamba anataka kujiunga na Tottenham. (Mail on Sunday)
Real Madrid wameafikia makubaliano na mchezaji mwenye umri wa miaka 22 raia wa Uholanzi Donny van de Beek, lakini bado hawajakubaliana kuhusu dau la uhamisho huo na klabu yake Ajax.. (Marca)
Mkufunzi wa Leicester City Brendan Rodgers anapanga kumnunua beki wa Norway Kristoffer Ajer, 21 kwa dau la £21m. (Star Sunday)
Barcelona wameafikia makubaliano na Real Betis kumsaijili beki wa Uhispania mwenye umri wa miaka 22Junior Firpo kwa dau la £22m. (ESPN)
MaoniMaoni Yako