Tanasha: Haijalishi ikiwa Diamond ana sifa ya wanawake, nataka watoto wengi naye


Mwimbaji wa Kitanzania Diamond Platnumz na mpenzi wake Mkenya Tanasha Donna.
Ikiwa ni mwezi mmoja tu umesalia kabla ya kujifungua mtoto wake wa kwanza, mwimbaji na mtangazaji wa redio Tanasha Donna tayari anafikiria kupata watoto wengi zaidi na mpenzi wake wa kitanzania, Diamond Platnumz.Akiongea wakati akiwajibu mashabiki wake kwenye ukurasa wake wa Instagram, Tanasha alifafanua kuwa yuko tayari kuzaa mtoto mwingine kwa Diamond.

"Labda mtoto wangu akiwa na umri wa miaka 5 hadi 7 basi tunaweza kufikiria, Tanasha alisema.Shabiki mwingine alitaka kujua ikiwa Tanasha haogopi kuachwa na Diamond, ambaye ni mvunjaji wa moyo wa siri.


Lakini katika majibu yake Tanasha alisema hatamuhukumu Diamond kwa yale yote ya zamani, bora tu ikiwa anamtendea haki."Kila mtu ana mahusiano ya nyuma, kila mtu anayo ya kale ,mimi kabla nimjue  Diamond nilishawaji kua na wapenzi. Nilikuwa na wapenzi watatu tofauti kabla kwahiyo siwezi kumhukumu mtu kulingana na zamani zao. Mimi naangalia mtu vile uko sasa hivi, ikiwa unanitendea sahii basi sisi hatuna shida, alisema Tanasha ambaye aliwahi kuwa na uhusiano na muigizaji wa Kenya Nick Mutuma
MaoniMaoni Yako