Taifa Stars Yailaza Kenya Kwa bao 4:1 na Kusonga mbele Michwano ya CHAN

Taifa Stars Yailaza Kenya  Kwa ba 4:1

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imesonga mbele baada ya kuitoa Harambee Stars kwa penalti 4-1 katika mchezo wa marudiano kusaka nafasi ya kufuzu Chan, uwanjani Moi Kasarani


TIMU ya Tanzania imeshinda dhidi ya Kenya kwa mikwaju ya penalti 4-1 baada ya dakika 90 kumalizika suluhu na kusonga mbele kwenye harakati za kufuzu CHAN.

Wafungaji wa Tanzania Erasto Nyoni, Paul Godfrey, Gadiel Michael, Salim Aye huku kipa watanzania Juma Kaseja akipangua mkwaju wa penalti.

Katika mechi ya awali timu hizo zilitoka suluhu Jijini Dar es Salaam katika mchezo ambao Stars ilitawala kwa kila kitu.
MaoniMaoni Yako