Taifa Stars kukipiga na Sudan

Taifa Stars kukipiga na Sudan

TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imefuzu hatua ya pili baada ya kuifunga Kenya kwa penalti 4-1 ikiwa ni mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (Chan) na sasa watakutana na Sudan.
Mechi hiyo iliyochezwa uwanja wa Moi Kasarani jijini hapa ilimalizika kwa sare tasa katika dakika 90 ambapo mchezo wa awali uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam timu hizo zilitoka sare tasa.
Mechi inayofuata ya Stars itachezwa Septemba 20 mwaka huu ambapo Stars wataanzia nyumbani.
Hata hivyo mechi hiyo pengine isingekwenda kwenye mikwaju ya penati ikiwa John Bocco angetumia vyema nafasi aliyopata dakika ya lala salama.
Bocco alinasa mpira uliomponyoka kipa wa Kenya, John Oyemba lakini nahodha huyo wa Taifa Stars akiwa analitazama lango, alipiga shuti hafifu lililopaa na kuinyima nafasi timu yake kupata ushindi.
Stars imefuzu hatua inayofuata kwa penaliti 4-1 ambapo penalti za Stars zilipigwa na Paul Godfrey 'Boxer', Erasto Nyoni, Gadiel Michael na Salum Aiyee.
MaoniMaoni Yako