" Siwataki Liverpool " :Unai Emery

Tokeo la picha la unai emery
Unai Emery amekiri kwamba asingependa kucheza dhidi ya Liverpool msimu huu lakini amesisitiza kwamba Arsenal watakuwa na hali ya chanya pindi watakapokabiliana na mabingwa wa Ulaya dimba la Anfield .

" Kwa sisi , tusingependa kucheza dhidi ya Liverpool, kamwe . Tusingependa kucheza dhidi yao . Hiyo ni changamoto yetu, mtihani mkubwa kabisa , kwa mashabiki , kwa sisi wote ,kwenda Anfield ukiwa tayari na Pointi sita ni nzuri sana ."


" Tutajiandaa kwa kuzuia na kushambulia na itabidi tujiandae jinsi gani ya kukabiliana na wachezaji wao watatu wa mbele baada ya hapo ndio tuukamate mchezo ."
MaoniMaoni Yako