SIMBA YASHAURIWA KUMTUMIA SHOBOUB ZAIDI KATIKA ADHABU, MASHAMBULIZI...Meneja wa Al Hilal, Mohamed Haroun amesema Simba itafaidika zaidi kama itampa nafasi kiungo Shiboub kucheza kama kiungo wa ushambulizi zaidi.

Haroun ambaye amefanya kazi na Shiboub kwa zaidi ya miaka minne amesema Shiboub ni mzuri sana anapokuwa anashambulia kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kutoa pasi za mwisho lakini kufunga pia. "Anajua afanye nini anapokuwa na mpira, anaweza kutoa pasi ya bao au kufunga. " Simba waendelee kumtunia katika mashambulizi ingawa siku akicheza kiungo cha ulinzi hawatakubali acheze mwingine, " alisema.

Tayari Shiboub amekuwa gumzo kutokana na uwezo wake aliouonyesha akiwa na kikosi cha Simba akitokea Al Hilal ya kwao Sudan.
MaoniMaoni Yako