Sunday, August 11, 2019

Simba yakumbuka waliokufa ajali ya moto

Tags

Simba yakumbuka waliokufa ajali ya moto


PAMBANO la Simba na UD Songo limeanza huku wawakilishi hao wa Tanzania wakivaa vitambaa vyeusi mkononi kuashirikia msiba wa kitaifa uliotokana na ajali ya moto iliyopoteza uhai wa watu karibu 100.
Ajali hiyo iklitokea asubuhi ya leo eneo la Msamvu, Morogoro baada ya lori ya mafuta kuanguka na wananchi kulikimbilia kuzoa mafuta kabla ya wengine kutaka kuiba betri na kusababisha moto uliowateketeza kila aliyekuwa amebeba dumu la mafuta.
Simba ipo mjini Beira, kuvaana na wenyeji wao UD Songo na mpaka sasa ikiwa inaingia dakika ya 10 matokeo yakiwa 0-0 lakini kabla ya kuanza, Simba walivaa vitembaa vyeusi kuomboleza vifo hivyo.