Simba yajipa angalizo kuelekea mchezo wa kimataifa dhidi ya UD Songo

MEDDIE Kagere mshambuliaji wa Simba, ametoa tahadhari kwa wachezaji wenzake akisema kwamba hawatakiwi kuwachukulia kirahisi wapinzani wao UD do Songo.

Simba itamenyana na UD Songo kwenye mchezo wa marudio kati ya Agosti 23-25 jijini Dar baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Msumbiji.


Msimu uliopita kwenye michuano ya kimataifa, Kagere alitupia mabao sita ana kazi ya kufanya pamoja na wachezaji wake kwenye mchezo wa marudio ili kusonga mbele.

“Kuelekea mchezo wa marudio tunatakiwa kuwa makini na kuchukulia kwa uzito mkubwa pambano ambalo tutachezwa kwani mashabiki pamoja na uongozi unahitaji matokeo," amesema.
MaoniMaoni Yako