Saturday, August 17, 2019

Simba Nooma Yajipigia Matajiri Wa Dar, Azam Fc Na Kutwaa Ngao Yao Ya Jamii Taifa

Tags

MECHI ya 12 leo Uwanja wa Taifa imekamilika na umezalisha mabao mengi kuliko mchezo wowote tangu kuanza kwa michuano hii mwaka 2001.

Sasa Simba imefikia hatua ya Yanga ambao walitwaa mataji hayo mara tano na leo wamefikia hatua ya kutwaa mataji matano.

Azam ambayo imecheza michuano hii mara sita imetwaa taji hilo mara moja sawa na Mtibwa Sugar na iliifunga Yanga kwa penalti.

Hivyo kwa sasa ni rasmi Pazia la Ligi Kuu Bara limefunguliwa kwa Simba kutwaa ngao yao ya jamii ambayo msimu uliopita walitwaa mbele ya Mtibwa Sugar kwa ushindi wa mabao 2-1.

Mabao ya Simba yamefungwa na Sharaf Shiboub ambaye alipachika mabao 2 dakika ya 17 na 21 la tatu limepachikwa na Chama dakika ya 56 na msumari wa mwisho umepachikwa na Kahata dakika ya 78.

Yale ya Azam yamepachikwa na Idd Chilunda dakika ya 13 na Frank Domayo dakika ya 78.