Simba Dimbani Leo KUwavaa UD Songo

Image

Mabingwa wa Tanzania Simba sc leo watakua dimbani kuitetea tiketi yao ya kuendelea kusonga katika hatua inayofuata ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwenye mchzo wa mkondo wa pili utakaopigwa jioni ya leo jijini Dar es salaam.

Mabingwa hao watachuana na UD Songo ya msumbiji huku ikihitaji ushindi kwani katika mchezo wa awali timu hisi zilitoka dimbani kwa sale tasa (0-0)

Kuelekea mchezo huo kocha mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kutafuta ushindi kwenye mchezo huo.

"“Tupo tayari na tunajua tunataka kushinda, tutafanya kila kitu kufanikisha hilo na wachezaji wanajua hilo. Tunatakiwa kuwa makini, tunajua tunakutana na timu nzuri na utakuwa mchezo mgumu lakini TUNAJIAMINI”
Patrick Aussems
MaoniMaoni Yako