Shikalo, Molinga waipa Yanga presha

Shikalo, Molinga waipa Yanga presha
Shikalo, Molinga waipa Yanga presha
WAKATI mashabiki wa Yanga, wakihesabu saa kabla ya kuishuhudia timu yao kesho ikishuka dimbani katika mchezo wa raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers, mabosi wa klabu hiyo wanahaha kusaka leseni za nyota wao watatu.
Kipa Farouk Shikalo, beki Mustapha Suleiman na straika David Muringa 'Ndama', leseni zao kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) bado hazijafika Jangwani na mabosi wao sasa wanapambana kufuatilia ili waweze kuwa miongoni mwa nyota watakaowakilisha nchi.
Yanga inatarajia kushuka dimbani saa 12 jioni kesho katika mchezo  huo na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Dismas Ten alisema leseni za wachezaji wengine wote zimetumwa isipokuwa nyota hao tu.
"Tunaendelea kupambana na tupo katika hatua nzuri za mawasiriano na viongozi wa CAF hadi jioni tutakuwa tumefanikiwa kupata leseni hizo na wachezaji wetu watakuwa katika kikosi chetu," alisema.
"Sababu za kukosekana kwa leseni hizo huku nyingine zikipatikana na kutokana na kuchelewa kwa usajili wa nyota hao lakini imani ya kuwanao katika mchezo wa kesho ipo palepale," alisema Ten.
Katika hatua nyingine ameomba mashabikinwa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao katika mchezo wao huo kwa  kuwahaikishia kuwa nyota wao wapo vizuri wana ari ya mchezo.
"Kwa mujibu wa daktari nyota wote wapo katika hari nzuri hakuna majeruhi hata mmoja japo vipimo vya mwisho anatarajia kuvimalizia jijini Dar es Salaam leo," alisema.