Saturday, August 17, 2019

Serikali Kufungua Tawi La Yanga Leo, Kocha Zahera Kupewa Tuzo

Tags

Serikali Kufungua Tawi La Yanga Leo, Kocha Zahera Kupewa Tuzo


JOKATE Mwegelo anayeiwakilisha serikali kama Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Tawi la Yanga, Mlipo Tupo lililopo Kisarawe mkoani Pwani.

Jakate atazindua tawi hilo lenye wanachama zaidi ya 100 ambalo litakuwa la kwanza kuzinduliwa Kisarawe.

Katibu wa tawi hilo, Abdallah Muga amesema kuwa pamoja na uzinduzi wa tawi hilo kutakuwa na zoezi la ugawaji wa kadi kwa wanachama wapya na kusajili wapya na kumtunuku Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera nishani ya uvumilivu kwa kuiongoza timu hiyo msimu uiopita.

"Tumewaalika viongozi mbalimbali wa ngazi ya juu lengo likiwa ni kumpa kocha Zahera tuzo ya nishani kwani msimu uliopita wakati kikosi kikiwa kwenye hali mbaya yeye alipambana na matarajio yetu mgeni rasmi awe Mkuu wa Wilaya, Jokate Mwegelo," amesema.