Sarri Asumbuliwa Na Ugonjwa Ya Mapafu


Klabu ya Juventus imethibitisha kocha wao mpya Maurizo Sarri anaumwa ugonjwa wa Pneumonia baada ya kufanyiwa vipimo.

Sarri,60, alikosa mechi ya kirafiki wikiendi iliyopita dhidi Triestina kwa kusumbuliwa na mafua, lakini baada ya kufanyiwa vipimo zaidi,imegundulika anaumwa Pneumonia.

Pneumonia ni maambukizi ambayo yanaweza kusababisha mapafu kujaa majimaji au usaha, na pia huleta homa ,baridi kali, na kupumua kwa shida.

Juventus ambao watafungua msimu mpya wa Serie A jumamosi hii dhidi ya Parma, wamethibitisha tayari kocha huyo ashaanza kupatiwa matibabu
MaoniMaoni Yako