Samatta, Mambo Magumu Genk

MAMBO yapo ovyo. Ndivyo unavyoweza kusema kwa Mbwana Samatta na chama lake la Genk KRC baada ya jana tena kunyukwa mabao 2-0 nyumbani na Zulte-Waregem, ikiwa ni mara ya pili mfululizo tangu kuanza kwa Ligi Kuu ya nchi hiyo, Jupiler League. 
Samatta, Mambo Magumu Genk

Watetezi hao wa ligi hiyo walinyooshwa kwenye Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, ambapo straika huyo wa kimataifa wa Tanzania na Mfungaji Bora wa timu msimu uliopita, alicheza kwa dakika zote 90 jana lakini kwa mara nyingine akashindwa kufunga.
Mabao yaliyoizamisha Genk jana yalifungwa na washambuliaji Mnorway, Henrik Rorvik Bjordal dakika ya sita na Mrundi, Saido Berahino dakika ya 78.
Samatta na timu yake walifungwa mabao 3-1 KV Mechelen katika mechi ya ufunguzi wa ligi hiyo iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa AFAS- Achter de Kazerne mjini Mechelen.
Katika mchezo huo, Samatta alifunga bao lake la kwanza la msimu huu, lakini haikusaidia kuepuka kulala kwa wenyeji wao.
MaoniMaoni Yako