Sababu ya mchezo wa Azam fc na Simba kubadilishiwa uwanja yatajwa

Sababu ya mchezo wa Azam fc na Simba kubadilishiwa uwanja yatajwa
HIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetaja sababu kubwa iliyofanya kuurejesha mchezo wa ngao ya jamii kati ya Simba na Azam FC uwanja wa Taifa ni ya kiufundi.

Awali mchezo huo maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza kati ya Agosti 23 ulipangwa uchezwe uwanja wa Samora, Iringa na leo taarifa imetolewa kwamba mchezo utachezwa uwanja wa Taifa.

Wilfred Kidao, Katibu Mkuu wa TFF amesema kuwa sababu kubwa ambazo zimefanya kubadilishwa kwa uwanja ni za kiufundi hivyo hawakuwa na namna ya kufanya.
MaoniMaoni Yako