"Ruvu Shooting bingwa mwaka huu" – Jeuri ya Masau Bwire baada ya kuifunga Yanga (VPL - 28/8/2019)


Baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Yanga na Ruvu Shooting Afisa habari wa klabu ya Ruvu Shooting,Masau Bwire ametamba juu ya matokeo walioyapa na kudai kua huo ndio mwanzo wa wa kaulimbiu yake ya papasa Square kwa msimu huu.

Tuko vizuri saana musimu huu, nilizungumza jana watu wakasema ni porojo tu, ni maneno tu na niliwaahidi nikasema mwaka huu Papasa Squared haina utani.


Aidha masau ameonesha kutoridhishwa na maamuzi baada ya goli lao la pili kukataliwa  kutokana na mfungaji kuotea.


Niwambie sasa hii ndi Ruvu Shootini, Tunachoomba niwaombe wataalamu wajaribu kulitazama lile goli  tulilofunga tukaambiwa kwamba ni offside. Tunachohitaji ni haki ile, Nilimsikia mwenyekiti wa kamati ya waamuzi Mzee wangu Chama, akisema hivi Mwamuzi ambaye timu itakua imefunga goli la wazi akawanyima huyo akavue samaki, Mwamuzi ambaye atawapa goli lisilo la haki akawapa timu kwa sababu zake anazozijua huyo pia akalime, mpunga, sijui akalime nini au akavue samaki.

Bwire ameahidi kuwa kama sheria 17 za soka zitafuatwa basi Ruvu Shooting ndio mabingwa wa ligi kuu Vodacom Tanzani Bara.

Sasa ninaomba   wataalamu walitazame hili goli, wathibitishe kweli kwamba ilikua ni offside au haikua offside basi yale aliyoyazungumza chama yaanzie hapa ili ligi yetu iwe nzuri. Maamuzi yakiwa mazuri, sheria 17 za mpira zikifuatwa, Ruvu Shooting mwaka huu Bingwa.
MaoniMaoni Yako