Ronaldo afichua siri yaushangiliaji wake


Ronaldo afichua siri yaushangiliaji wake
TURIN, ITALIA. SI unaijua ile staili ya kushangilia la Cristiano Ronaldo? Sasa je unajua ilianzia wapi? Straika huyo amefunguka kwamba aliianzisha kwa mara ya kwanza baada ya kuwatungua bao Chelsea.

Straika huyo Mreno hivi sasa anajulikana kwa aia yake hiyo ya ushangiliaji ambayo huruka juu na kugeuka kabla ya kurudisha mikono kwa nyuma huku akimalizia na ukulele wa "Sii" – kila anapofunga goli.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34 aliitumia staili ya ushangiliaji mara 21 akiwa na Juventus kwenye Serie A msimu uliopita, lakini mashabiki wa soka wa nchini Marekani ndiyo waliokuwa wa kwanza kuishuhudia staili hiyo.

Akizungumza na YouTube ya Soccer.com, mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon D'or alibainisha aliitumia staili hiyo kwa mara ya kwanza wakati akichezea Real Madrid katika mechi ya kirafiki dhidi ya Chelsea.

"Ndiyo, nilikuwa Marekani na tulikuwa tukicheza dhidi ya Chelsea na sijui ilitokea wapi. Nilifunga tu goli na kisha kusema, 'sii!'" anakumbuka.

"Lakini ilikuwa tamu sana, niwe muwazi.
MaoniMaoni Yako