Monday, August 12, 2019

Ronaldo aanza kuchunguzwa na polisi

Tags

POLISI wa Korea Kusini wameanza kufuatilia suala la Cristiano Ronaldo kugomea kucheza mechi ya kirafiki kati ya Juventus dhidi ya Kombaini ya mastaa wanaocheza Ligi Kuu Korea Kusini.

Mechi hiyo ilichezwa Julai 26 mwaka huu ambalo Ronaldo aligoma kucheza licha ya mkataba kudai kwamba angecheza.

Promota wa mchezo huo aliahidi kuwa atacheza jambo lililofanya mashabiki wengi kununua tiketi ambazo zilikuwa bei ghali.

Mashabiki walivamia ofisi za promota huyo wakitaka watajiwe sababu kwa nini nyota huyo hajacheza jambo lililofanya Polisi waweke usawa na kuwataka mashabiki kufungua kesi.

Mahabiki hao wamefungua kesi Polisi ya ulaghai kutokana na kile walichoahidiwa kutokamilika.