Monday, August 12, 2019

Rollers: muziki wa Yanga sio wa kitoto, tunajipanga kupata matokeo

Tags

Rollers: muziki wa Yanga sio wa kitoto, tunajipanga kupata matokeo
Rollers: muziki wa Yanga sio wa kitoto, tunajipanga kupata matokeo
KOCHA Mkuu wa Township Rollers,Thomas Truch, Kocha Mkuu wa Township Rollers amesema kuwa kikosi chake kina kazi ngumu ya kufanya mbele ya Yanga baada ya kukubali kupata sare ya kufungana bao 1-1.

Rollers ilikubali kupata sare ya kufungana na kikosi cha Yanga bao 1-1 uwanja wa Taifa licha ya kuanza kupachika bao la kuongoza mapema dakika ya 7 kwenye mchezo wa awali Ligi ya Mabingwa.

"Tumewatambua wapinzani wetu namna walivyo na mbinu za kutafuta matokeo kwani licha ya kuwabana mwanzo kwa kuwafunga hawakukata tamaa waliendelea kutuandama na mwisho wa siku wakapata walichokitaka.

"Sina hofu kubwa sana japo ninapaswa kujipanga vema kwani nacheza na timu ambayo ina wachezaji wenye kiu ya kupata ushindi hivyo sipaswi kuwabeza hata nikiwa nyumbani," amesema.