Monday, August 5, 2019

Rasmi Okwi Awaaga Mashabiki Na Uongozi Wa Simba

Tags

Rasmi Okwi Awaaga Mashabiki Na Uongozi Wa Simba
EMMANUEL Okwi, nyota wa zamani wa Simba na sasa amesema kuwa daima atawakumbuka mashabiki na viongozi wa Simba kwa upendo walioonyesha kwake.

Okwi mkataba wake na Simba umemalizika na sasa yupo na timu ya Itthadalexsc leo amewaaga rasmi mashabiki wake wa Simba ambapo amesema:- "Napenda kuwashukuru kwa sapoti ya muda mrefu na kumbukumbu nzuri ambazo tumezifanya kwa pamoja na kwa miaka mingi, muda mwingi.

"Muda wote mmekuwa mkinifanya sehemu ya familia na ninawakubali katika hilo na kuheshimu pia upendo wenu

"Nina kila sababu za kuwashukuru viongozi wangu wa benchi la ufundi na uongozi kwa ujumla namna ambavyo wamekuwa wakipenda kuona tunafikia malengo.

"Kwa sasa nipo Itthadalexsc daima nitawakumbuka kwa moyo mmoja Simba ndani ya moyo kwani ni nguvu moja," amesema.

Msimu wa mwaka 2018/19, Okwi alifunga mabao 15 na aliweka rekodi ya kufunga hattrick mbili ndani ya Ligi Kuu ambayo haikuvunjwa mpaka msimu unameguka.