RASMI BOCCO KUIKOSA UD SONGONahodha wa timu ya Simba, John Bocco ndiye mchezaji pekee aliye thibitishwa kuwa hataweza kucheza mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo siku ya Jumapili katika uwanja wa Taifa


Bocco alipata majeraha katika mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Azam FC, Jumamosi iliyopita ambapo mpaka sasa yupo chini ya uangalizi wa madaktari na hajaanza mazoezi mpaka sasa


Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu amesema kuelekea mchezo huo wachezaji watatu waliokuwa majeruhi wamerejea mazoezini na sasa Bocco pekee ndiye majeruhi


"Mpaka sasa Bocco ndiye hatakuwa sehemu ya mchezo wetu wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo lakini Aishi Manula, Ibrahim Ajibu na Wilker Henrique Da Silva wamerejea na wanafanya mazoezi na wenzao," alisema Rweyemamu
MaoniMaoni Yako