Saturday, August 17, 2019

Polisi Tanzania Yachekelea Kuinyoosha Yanga

Tags

Polisi Tanzania Yachekelea Kuinyoosha Yanga



DITRAM Nchimbi, mchezaji wa Polisi Tanzania amesema kuwa ushindi wao mbele ya Yanga ni mwanzo mzuri kwa kikosi hicho kuelekea kwenye msimu mpya unaotarajiwa kuanza Agosti 23.


Nchimbi, jana alifunga bao la pili kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Ushirika Moshi na lile la kwanza lilipachkwa na Marcel Kaheza.


Nchimbi amesema kuwa:"Kupata ushindi mbele ya Yanga ni mwanzo mzuri kwetu kwani unatufanya tuzidi kujiamini na kuongeza nguvu kwa ajili ya msimu mpya, hivyo kikubwa kwetu ni kuendelea kujipanga kufanya vizuri zaidi," amesema.